Mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 6,314,477,066.00 unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya umwagiliaji unahusisha ujenzi wa banio na tuta, ujenzi wa mfereji mkuu, ujenzi wa mfereji wa upili, ujenzi wa mfereji wa matupio, ujenzi wa barabara za mashambani, ujenzi wa vivusha maji, na ujenzi wa ofisi ya mhandisi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tunduru, ambao wamezoea mazingira ya kawaida ya kujifunza, sasa wanashuhudia mapinduzi ya elimu kwa kutumia Darasa Janja, zana mpya iliyoingia darasani na kuleta uhai mpya.Walimu wanatumia televisheni hizi janja kuonyesha masomo kwa njia ya video, picha, na michoro. Badala ya kutumia chaki na ubao pekee, walimu sasa wanaweza kuwapa wanafunzi uzoefu wa kujifunza unaovutia na unaowahusisha zaidi.
Kupitia makala maalum ya video ya maonesho ya Nanenane yaliyofanyika jijini Mbeya, tumeshuhudia bidhaa na ubunifu kutoka Tunduru,mazao ya kilimo, ufugaji bora, bidhaa zenye thamani zaidi, na maarifa ya kisasa ya kilimo.
Habari njema
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.