• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

ELIMU YA FURSA ZA KIUCHUMI ZAWAFIKIA VIJANA WA BODABODA, BAJAJI NA MAGUTA TUNDURU.

Imewekwa : February 7th, 2026

Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeendelea na ziara maalum za kutembelea vijiwe vya maafisa usafirishaji wa bodaboda, bajaji na maguta katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za Serikali za kuwafikia vijana moja kwa moja katika maeneo yao ya kazi, kuwapatia elimu, kusikiliza changamoto zao na kuwaunganisha na fursa mbalimbali za maendeleo.

Katika ziara hizo, wataalamu walitoa elimu kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo ndani ya Wilaya ya Tunduru, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, pamoja na fursa za mikopo ya vyombo vya moto kama pikipiki, bajaji na maguta inayotolewa na Benki za NMB na CRDB, kwa lengo la kuwawezesha vijana kumiliki vyombo vyao na kujitegemea kiuchumi.


Aidha, vijana walipatiwa taarifa kuhusu fursa za mafunzo ya muda mfupi ya udereva yatakayokuwa yakitolewa na Chuo cha Ufundi Nazareth Mbesa – Tawi la Tunduru Mjini (Biasi). Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha vijana kupata vyeti vya mafunzo ya udereva na kumiliki leseni halali, hatua itakayowawezesha kufanya kazi kama madereva rasmi wanaotambulika kwa mujibu wa sheria.

Katika kutekeleza adhma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwafikia na kuwasikiliza vijana, viongozi na wataalamu wa Halmashauri walisikiliza na kupokea changamoto pamoja na ushauri uliotolewa na vijana, ili kuzifanyia kazi na kuboresha mazingira yao ya kazi na maisha kwa ujumla.


Vilevile, elimu ilitolewa kuhusu huduma ya msaada wa kisheria kupitia Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign, inayotolewa bila malipo kwa wananchi, kwa lengo la kutatua migogoro katika jamii, kulinda haki za wananchi na kuwezesha maendeleo endelevu.


Katika ziara hizo, vijana pia walielimishwa kuhusu umuhimu wa kudumisha amani, upendo na mshikamano katika jamii, hususan kwa makundi ya watoa huduma za usafirishaji, ili kuhakikisha usalama, utulivu na maendeleo ya Wilaya ya Tunduru vinaendelea kudumishwa wakati wote.


Ziara hizi ni sehemu ya mpango endelevu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wa kuendelea kutembelea vijiwe vya bodaboda, bajaji na maguta, kama mkakati wa Serikali wa kuwafikia vijana moja kwa moja, kutatua changamoto zao na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kwa ustawi wa vijana na maendeleo ya wilaya kwa ujumla.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA NEST YAWAWEZESHA MAFUNDI WA NDANI, MAKUNDI MAALUM NA WAZABUNI KUSHIRIKI ZABUNI ZA SERIKALI.

    February 07, 2026
  • FURSA NA ELIMU YA KODI ZAWAFIKIA LOCAL FUNDI, MAKUNDI MAALUM NA WAZABUNI TUNDURU.

    February 07, 2026
  • ELIMU YA FURSA ZA KIUCHUMI ZAWAFIKIA VIJANA WA BODABODA, BAJAJI NA MAGUTA TUNDURU.

    February 07, 2026
  • WAZEE WATAJWA NGUZO YA MAENDELEO: MWENYEKITI HALMASHAURI YA TUNDURU AZUNGUMZA NA WAZEE WA WILAYA.

    February 04, 2026
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.