Miradi ya Maendeleo Inayoendelea kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2017/2018
SEKTA YA AFYA.
katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali inaendele na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya afya, ambayo ina michango ya fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali, ikiwa fedha zingine ni zile za miradi ya maendeleo kutoka serikali kuu, mchango wa mapato ya ndani (Own source), mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo, na fedha kutoka kwa wahisani.
1.Ujenzi wa kituo cha Afya Mkasale, mradi huu ni upanuzi wa majengo katika kituo cha afya mkasale ambapo jumla ya miloni 400 zitatumika katika ujenzi wa Nyumba ya Mganga, Wodi ya mama na mtoto, Maabara, Chumba cha Upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti,kichomea taka na placenter Pit kwa ajili ya kutupa uchufu baada ya kinamama kujifungua.
1.JENGO LA MAABARA.
Ujenzi wa Jengo la Maabara katika Ukarabati unaoendelea katika kituo cha Afya cha Mkasale Wilayani Tunduru.
2.JENGO LA NYUMBA YA MGANGA.
Jengo la nyumba ya mganga linaloendelea kujengwa katika kituo cha Afya Mkasale
3. JENGO LA MORTUARY
Jengo la Mortuary kituo cha afya Mkasale ni miongoni mwa majengo ya yanaendelea kujengwa.
UJENZI WA WODI MBILI HOSPITALI YA WILAYA.
2. Ujenzi wa wodi hospitali ya Wilaya, katika hospitali ya wilaya halmashauri inaendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa huduma za afya na kupitia mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2016/2017 serikali ilitenga shilingi milioni 150 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake na wanaume ili kupata sehemu ya kupumzikia kwa wagonjwa wa upasuaji kwani hapo awali walikua wananchanganywa kwenye wodi za wagonjwa wa kawaida hali ambayo ni hatarishi kwa afya zao.
UJENZI WA KITUO CHA AFYA NAKAYAYA.
3.Ujenzi wa kitu cha Afya Nakayaya- mradi unafanyika kwa ushirikiano wa wadau wa maendeleo, mkuu wa wilaya na ofisi ya mkurugenzi mtandaji ili kuweza kupunguza changamoto ya mlundikano wa wagonjwa katika hospitali ya wilayakwani idadi ya wananchi wanaongezeka hivyo hospitali kulemewa.
Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Nakayaya ulianza mwaka 2016 kwa mchango ya wafanyabishara na wadau mbalimbali waliouguswa na mipango ya utekelezaji wa seriakali ya awamu ya Tano wa Kuboresha Huduma za Afya.
Ni baadhi ya majengo ya mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Nakayaya unaoendelea kutekelezwa, kwa mchango wa wadau mbalimbali kwa kushirikiana na serikali.
UJENZI WA NYUMBA YA MGANGA -ZAHANATI YA NAIKULA
Halmashauri katika mwaka wa fedha 2017/2018 ilitenga fedha kiasi cha shilingi milioni 30,000,000. kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi ya moja kwa mbili katika zahanati ya Naikula kupitia fedha za makusanyo ya ndani. Ujenzi huo upo katika hatua ya umaliziaji wa ujenzi wa stoo, jiko, bafu na vyoo.
Jengo la Nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Naikula Kata ya Namasakata.
UJENZI WA ZAHANATI KIJIJI CHA LEGEZAMWENDO.
Mradi wa ujenzi zahanati katika kijiji cha Legezamwendo ulinza mwaka wa fedha 2011/2012, kwa kutumia fedha za Ruzuku ya Maendeleo ya Halmashauri, hadi kufikia sasa mradi huu umegharimu jumla ya milioni 120,000,000. ujenzi huu baadhi ya majengo yamekamilika na mengine yanaendelea kujengwa kulingana na upatikanaji wa fedha.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.