Mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima na wadau wa masoko ya mazao. Mfumo huu umesaidia kujenga uhusiano mzuri na wa haki kati ya mkulima na mnunuzi wa mazao. Kabla ya mfumo huu, kulikuwa na unyonyaji ambapo wakulima walikuwa wanauza mazao yao kwa bei ya chini sana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitoa kauli hii katika mkutano wa jukwaa la mifumo ya chakula Africa (AGRF 2023). Alisisitiza kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani umekuwa kiunganishi kizuri baina ya wakulima na soko, na umesaidia kuondoa unyonyaji uliokuwepo hapo awali.
Mfumo huu umewaletea manufaa makubwa wakulima, hasa katika Wilaya ya Tunduru. Kwa msimu huu, mkulima wa ufuta ameweza kuuza kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kwa kilo moja, na mkulima wa mbaazi ameweza kuuza si chini ya shilingi 1,500 kwa kilo moja. Hii ni bei nzuri na inawawezesha wakulima kupata faida kubwa zaidi.
Serikali chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe, Dkt.Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za kuboresha miundombinu na mifumo ya kuwezesha mfumo huu wa stakabadhi ghalani. Hatua hizi ni muhimu ili kuhakikisha kuwa kuna muunganiko mzuri baina ya mkulima na mnunuzi wa mazao. Hatua hizi zitawasaidia wakulima kupata masoko bora zaidi na kuondokana na unyonyaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa Wilaya zinazoongoza katika kilimo cha zao la Korosho,Ufuta na Mbaazi. Jitihada zake za kuboresha kilimo, kutoa Elimu kwa wakulima, kuimarisha masoko ya ndani na nje zimeleta mafanikio makubwa na kuleta maendeleo ya kiuchumi.
TUME ya Taifa ya Mpango wa matumizi bora ya ardhi (National Land Use Planning Commisio-NLUPC) imeendesha zoezi la kupendekeza, kutathmini na upimaji wa ardhi kwa matumizi mbalimbali katika Wilaya ya Tunduru.
Mpango huu wa Tume umepitia katika vijiji nane katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambavyo ni kijiji cha Muhuwesi, Liwangula, Ngapa,Chawisi, Mnazi mmoja,Matemanga,Ligunga na Jaribuni.
Lengo la zoezi hilo ni kuboresha matumizi ya ardhi nchini kwa kuweka mpango madhubuti unaolinda na kusimamia rasilimali ardhi kwa ajili ya matumizi endelevu. Zoezi hili litasaidia kukabiliana na migogoro ya ardhi baina ya watumiaji mbalimbali, vile vile kuwezesha upatikanaji wa Ardhi kwaajili ya uwekezaji katika maeneo hayo.
Akizungumza Bi Pili Msati ,Msimamizi wa kanda nyanda za juu Kusini -(NLUPC), alisema , lengo la Serikali ni kujenga uelewa kwa wananchi wa maeneo ambayo yana muingiliano wa matumizi ya ardhi ,ili kuweka matumizi bora na sahihi ya ardhi kwa watumiaji tofauti.
"Tume imekuja kuwezesha mipango kwa lengo la kuweka sawa wastani wa matumizi ya ardhi,lazima tuhakikishe kwamba wananchi wanaishi kwa kuheshimu hifadhi na sehemu zote za ardhi zilizotengwa kwa matumizi maalumu”. Alisema.
Aidha Mpima Ardhi (W) Tunduru Ndg. Jeremia Nhambu, ameishukuru Serikali kwa kuleta mpango huu, kwani litasaidia kukabiliana na migogoro ya matumizi ya ardhi baina ya watumiaji mbalimbali hasa ya wafugaji na wakulima kwa njia ya Amani na haki. Pia, ameongezea kwa kuwakaribisha wawekezaji kwani mpango huu unaainisha maeneo ya uwekezaji katika maeneo yaliyoainishwa.
Pia kwa upande wao wananchi wa vijiji vilivyopitiwa na mpango huo ,wameishukuru Serikali kwa mpango huo kwani utapunguza migongano kati ya wakulima na wafugaji, pia wamehaidi kulinda na kufuata mpango huo wa Matumizi Bora ya Ardhi.
Mpango mzuri wa matumizi ya ardhi unaweza kuvutia wawekezaji kwa kutoa mwongozo wa maendeleo ya muda mrefu. Hii inawahakikishia wawekezaji kuwa siasa ya ardhi za eneo hilo ni thabiti na ina misingi ya kisheria, ambayo inaongeza Imani yao katika uwekezaji.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imefanya mkutano maalumu wa kufunga hesabu za fedha kwa mwaka 2022/2023, kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa inayozitaka Halmashauri nchini kufunga hesabu na kuwasilisha kwa mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mh. Hairu Mussa alisema, Halmashauri ilikusanya kutoka vyanzo vyake (own source) zaidi ya shilingi bilioni 4.3 ambayo ni sawa na asilimia 93 ya makisio ya mwaka shilingi bilioni 4.7.
Kutokana na utekelezaji mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo, rasilimali za muda mrefu na mfupi za Halmashauri zimepanda thamani toka zaidi ya shilingi milioni 65 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia zaidi ya shilingi milioni 70 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
“Mapato tunayokusanya tunahakikisha ,yanaenda katika atekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yetu ya kata na vijiji kuboresha huduma za jamii”
Akifafanua taarifa hiyo, ndugu Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Tunduru ndugu Masanja Kengese, amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha fedha shilingi bilioni 4.8.
“Rai yangu kwa waheshimiwa madiwani kuweza kushirikiana na halmashauri katika kudhibiti mapato, ukizingatia mapato ya halmashauri ya wilaya ya Tunduru yanapatikana kupitia mazao, hivyo, tunawaomba waheshimiwa madiwani kusaidia kudhibiti utoroshaji wa mazao”.
Alisema.Wakizungumza kwa nyakati tofauti waheshimiwa madiwani Said Kiosa(kata ya Nanjoka) na Daudi Amlima (kata ya Nakayaya) wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Wilaya ya Tunduru.
Halmahauri ya wilaya ya Tunduru ina Tarafa 7 ,kata 39 ,vijiji 157 na vitongoji 1179 ,Serikali ya Halmashauri ya wilaya ya Tunduru inahakikisha maeneo yote yanafikiwa na huduma za jamii kupitia mapato ya ndani na mapato kutoka Serikali kuu.
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.