D. KAMATI YA KUDUMU YA KUDHIBITI UKIMWI.
Majukumu ya Kamati
1. Kushirikisha wadau tofauti katika maeneo husika ili kuongeza uchangiaji wa mawazo na/au nyenzo, usimamizi, uratibu na utekelezaji wa kazi za Tume za kudhibiti UKIMWI.
2. Kusimamia uundaji wa Kamati zote za kudhibiti UKIMWI.
3. kupendekeza na kuchambua hali ya UKIMWI/Mipango na utekelezaji wake na kufikisha katika ngazi husuka kwa hatua zaidi;
4. Kutathmini hali ya UKIMWI katika eneo lake kuhusu;
(i) Idadi ya waathirika: wagonjwa, yatima, wajane;
(ii) Kasi ya maambukizo;
(iii) Mazingira Maalum yanayochangia maambukizo;
(iv) Uelewa wa wananchi juu ya janga hili.
5. Serikali haitatoa fedha kwa Halmashauri isiyokuwa na mipango madhubuti ya kudhibiti UKIMWI.
6. Kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule anafanya hivyo.
7. Kuweka mikakati ya makusudi juu ya njia bora za kuchangia baadhi ya huduma za Elimu na Afya.
8. Kubuni na kupendekeza njia bora za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya milipuko.
9. Kupendekeza Sheria Ndogo za Kamati hii.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.