Timu ya Wakaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, chini ya uongozi wa Mkuu wa Kitengo Ndugu Imani Bukulu, inaendelea kwa kasi na jukumu lake la kila siku la ukaguzi. Jukumu hilo linahusisha kufuatilia na kurekebisha hoja za ukaguzi zilizotolewa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Jukumu kuu la timu hiyo kwa sasa ni kufanya mapitio ya kina ya mpango kazi wa utekelezaji wa hoja za CAG, kwa kutumia Mfumo wa Ufuatiliaji wa Hoja za Kikaguzi (IFT-MIS - Inspection and Financial Tracking Management Information System). Mfumo huu ni muhimu kwa sababu unawezesha kufuatilia utekelezaji wa hoja za ukaguzi kwa uwazi na ufanisi, na kuhakikisha kuwa mapungufu ya kifedha na kiutawala yanarekebishwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, matumizi ya mfumo wa IFT-MIS yameboresha kwa kiwango kikubwa kasi na ufanisi wa ukaguzi, kwani nyaraka zote hupatikana kidigitali, jambo linalorahisisha uhakiki wa taarifa na kupunguza changamoto za upotevu wa nyaraka za karatasi.
Aidha, wakaguzi wamesisitiza kuwa ukaguzi wa mara kwa mara si tu unasaidia kugundua changamoto mapema, bali pia ni chachu ya kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wote wanaosimamia mapato na matumizi ya Serikali.
Kikao hicho, kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Denis Masanja, kiliwaleta pamoja Viongozi muhimu katika ngazi za utawala wa wilaya, walijumuisha watendaji mbalimbali wenye jukumu la kusimamia na kutekeleza sera za serikali katika ngazi ya wilaya.
Madhumuni makuu yalikuwa kuwajengea uelewa watendaji wa serikali kuhusu sheria, kanuni, na taratibu zinazopaswa kufuatwa katika masuala mbalimbali ya uongozi
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.