• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

RPC RUVUMA AZINDUA RASMI JENGO LA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO TUNDURU.

Imewekwa : February 9th, 2026

Wilaya ya Tunduru imepiga hatua muhimu katika kuimarisha ulinzi, usalama na utoaji wa haki katika masuala ya jinsia na watoto kufuatia uzinduzi rasmi wa jengo la Dawati la Jinsia na Watoto, uliofanyika leo tarehe 09 Februari, 2026.


Jengo hilo limezinduliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marko Chilya, ambaye amesema kuwa uwepo wa jengo hilo utarahisisha utoaji wa huduma za kisheria, ushauri na ulinzi kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto katika Wilaya ya Tunduru.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, SACP Marko Chilya amesisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kupinga vitendo vya ukatili, huku akibainisha kuwa Dawati la Jinsia na Watoto ni nyenzo muhimu ya kuhakikisha haki, usalama na ustawi wa makundi maalum yanalindwa ipasavyo.


Tukio hilo lilipambwa na watoto kutoka katika Shule za Msingi na awali za wilayani Tunduru, Aidha,watoto kutoka  Kituo cha Malezi ya Watoto Wadogo Mchana "Bright Future" walikua kivutio , ambapo walionesha ujumbe mbalimbali kupitia mabango yenye kaulimbiu zinazoelezea umuhimu wa uwepo wa Dawati la Jinsia na Watoto katika jamii, hatua iliyovutia hisia za washiriki wa hafla hiyo.

Uzinduzi wa jengo hilo unaonesha dhamira ya Serikali kupitia Jeshi la Polisi katika kuimarisha mazingira salama kwa wananchi wote, pamoja na kuhakikisha haki zao zinalindwa kwa vitendo, sambamba na malengo ya Taifa ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • RPC RUVUMA AZINDUA RASMI JENGO LA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO TUNDURU.

    February 09, 2026
  • NANDEMBO YAUNGANA KWA AMANI: WANANCHI WAPATIWA ELIMU YA UPENDO NA MSHIKANO KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII

    February 08, 2026
  • MAFUNZO YA MFUMO WA NEST YAWAWEZESHA MAFUNDI WA NDANI, MAKUNDI MAALUM NA WAZABUNI KUSHIRIKI ZABUNI ZA SERIKALI.

    February 07, 2026
  • FURSA NA ELIMU YA KODI ZAWAFIKIA LOCAL FUNDI, MAKUNDI MAALUM NA WAZABUNI TUNDURU.

    February 07, 2026
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.