Leo, tarehe 11 Februari, 2026, Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeendelea na mafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani, ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya mafunzo hayo yanayolenga kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao ya msingi ya kiuongozi na uwakilishi wa wananchi.


Mafunzo hayo yamelenga kuwapa Madiwani uelewa mpana kuhusu majukumu yao ya kisheria na kiutendaji, ili kuongeza ufanisi katika kusimamia maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika maeneo yao ya uwakilishi.
Kabla ya kuanza kwa mafunzo ya leo, Waheshimiwa Madiwani walisimama kwa dakika mbili kumkumbuka na kumuenzi marehemu Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Namasakata, Mhe. Rashidi Saidi Makosela, aliyefariki dunia tarehe 09 Februari, 2026, baada ya kupata ajali. Tukio hilo lilitokea siku ya kwanza ya mafunzo hayo, na limeacha pengo kubwa katika Baraza la Madiwani na kwa wananchi wa Kata ya Namasakata.

Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inaendelea kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wote wa Kata ya Namasakata kwa msiba huo mkubwa, huku ikisisitiza mshikamano na umoja katika kipindi hiki cha majonzi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.