1.0: UTANGULIZI.
Idara ya Elimu Msingi ni mojawapo kati ya Idara mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru. Idara hii ina vitengo vinne ambavyo vinaongozwa na Wakuu wa vitengo ambao wanamsaidia Afisa Elimu katika kutekeleza majukumu yake ya Idara ya kila siku. Vitengo hivyo ni Elimu ya watu wazima, Taaluma, Vifaa na Takwimu na Utamaduni na Michezo.
Kazi na majukumu ya kila kitengo yamefafanuliwa vizuri katika taarifa hii sehemu ya vitengo vilivyopo kwenye Idara. Ikumbukwe kwamba Idara ya Elimu Msingi ni moja ya Idara kubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, hivyo majukumu yake ni mtambuka ambayo yanagusa Idara nyingine kama vile, Afya, Maji, Maendeleo ya Jamii, Kilimo na Mazingira.
Idara inafanya shughuli zake kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizowekwa na TAMISEMI na Serikali kuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata Elimu bora itakayowawezesha kufaulu mitihani yao na kumudu maisha yao ya kila siku katika Nyanja mbalimbali. Idara ina Watumishi ambao wanaweza kutimiza malengo yaliyowekwa na Idara endapo watasimamiwa na kuwepo mazingira ya kufundishia ikiwemo miundombinu mfano, Vyumba vya Madarasa, Madawati, na Matundu ya Vyoo.
2.0 DIRA YA MWELEKEO
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imedhamiria kwamba kujenga uwezo wa kutoa huduma bora za Kijamii na Kiuchumi kwa watu wake kwa lengo la kuinua hali zao za kimaisha ifikapo mwaka 2025.
MWELEKEO
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imechukua hatua ya kuwawezesha watu wake kukuza Uchumi kwa lengo la kuboresha hali zao za kimaisha na kuongeza umri wa kuishi kutoka miaka 40 - 48 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
3.0: MALENGO YA IDARA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA.
- Kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule na kuwa na darasa la awali katika kila shule.
- Kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu
- Kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mimba na utoro.
-Kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la nne na darasa la saba katika mitihani yao.
-Kuondoa matatizo ya madawati, vyumba vya madarasa, nyumba za Walimu na matundu ya vyoo
-Kuanzishwa vituo vya MEMKWA katika shule mbalimbali ili kuwapatia Elimu watoto waliokosa Elimu katika Mfumo rasmi
-Kufuatilia ufundishaji katika shule zote zilizopo katika halamashauri ili kuona kama walimu:-
Wanajiandaa kabla ya kuingia darasani
Wanaingia darasani na wanafundisha
Wanatoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi
Wanafanya tathimini ya ufundishaji
Kuwa na uongozi wa shule ulio imara wenye uwezo wa kusimamia ufundishaji, nidhamu, ya Walimu na Wanafunzi na unaoshirikiana na kamati ya shule na jamii kwa ujumla katika maswala yanayohusu shule kama vile. Vikao, mapato ya shule, miradi ya miundombinu na mipaka ya shule.
Kutumia vituo vya walimu (Crusters) kwa ajili ya kufundisha mambo mabalimbali ya kielimu yakiwemo matumizi ya mitaala, Elimu nje ya Mfumo rasmi, usimamizi wa miradi ya shule, matumizi ya fedha zinazopelekwa na Serikali kwa ajili ya uendeshaji wa shule na ufundishaji wa mada ngumu.
Kukuza vipaji vya wanafunzi katika fani za utamaduni na michezo kwa kusimamia shughuli za utamaduni kama vile, ngoma, nyimbo, mashairi, ngonjera, maigizo na michezo mbalimbali inayofanyika katika shule zote.
Kila shule kuwa na mradi wa Elimu ya kujitegemea ambao utaongeza mapato ya shule na uhifadhi wa mazingira.
Kuwahudumia walimu na wananchi kwa usawa na kwa haraka wanapokuwa na mahitaji ya kuhudumiwa na Ofisi ya Elimu kama vile, uhamisho wa wanafunzi, ruhusa, ugonjwa na vifo, kujibu barua za walimu kwa haraka, kupitisha mihtasari ya matumizi ya fedha za shule, kusikiliza shida na matatizo ya walimu na kuwathamini.
Kutoa motisha kwa Walimu na Shule zilizofanya vizuri katika taaluma, michezo, usafi na utunzaji wa mazingira.
Kuwa eneo lisilopokea rushwa (Curruption Freezone) ambapo huduma itatolewa kwa haki bila upendeleo, kwa haraka na bila usumbufu.
Kushirikiana na wadau wa kisekta kama vile, Idara ya Elimu Sekondari, Ukaguzi wa Shule, Tume ya Utumishi wa Walimu na Chama cha Walimu Tanzania katika kusimamia utoaji wa Elimu bora na huduma bora kwa Walimu.
Kila mdau wa Elimu anapata taarifa za Idara ya Elimu bila vikwazo kwa usahihi na haraka zinapohitajika.
4.0: VITENGO VYA IDARA NA MAJUKUMU YAKE
Kama ilivyoelezwa katika utangulizi wa taarifa hii idara ina vitengo vinne (4) ambavyo ni.
Elimu ya Watu Wazima ambayo ndani yake kuna vitengo vidogo vitano (5) ambavyo ni vielelezo, ufundi, kilimo, Sayansi kimu na Elimu Maalum.
Taaluma
Vifaa na takwimu
Utamaduni ambacho ndani yake kuna kitengo kidogo cha michezo.
Idara inafanya kazi zake chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.