IFAHAMU IDARA YA MAZINGIRA NA UTHIBITI WA TAKA NGUMU
Idara ya Mazingira na Uthibiti wa Taka Ngumu ni mojawapo ya idara katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Idara ina mtumishi mmoja tu, ambaye kwa sasa ndio Mkuu wa Idara.
Majukumu ya Idara:
- Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali zinazohusu usimamizi na hifadhi ya mazingira
- Kutoa elimu ya hifadhi ya mazingira kwa wadau mbalimbali
- Kushiriki katika kuandaa mpango kazi na bajeti za idara
- Kushiriki katika tafiti zinazohusu usimamizi na uhifadhi ya mazingira
- Kufuatilia utekelezaji wa sera na sheria zinazohusiana na usimamizi wa mazingira
- Kufuatilia na kuanzisha maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa
- Kupitia na kushauri kuhusu taarifa za tathmini ya athari kwa mazingira (Environmental Impact
Assessment) na mpango mkakati wa tathmini ya mazingira (Strategic Environmental
Assessment)
- Kuandaa na kuratibu utekelezaji wa mikakati ya matumizi salama ya teknolojia ya kisasa
(Biosafety)
- Kufanya tathmini ya maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za kiuchumi zisizoendelevu
(kama vile uchimbaji wa madini, Kilimo, Ujenzi, Ufugaji n.k.)
- Kubainisha na kupendekeza masuala ya mazingira yanayopaswa kuhusishwa katika mipango
ya kisekta
- Kuratibu miradi mbalimbali inayohusu usimamizi na hifadhi ya mazingira
- Kupitia taarifa ya hali ya mazingira nchini (State of the environment report) na kutoa ushauri
- Kutoa ushauri kuhusu utekelezaji wa mikataba na maazimio mbalimbali ya Kitaifa, Kikanda na
Kimataifa kuhusu usimamizi wa mazingira
- Kufanya kazi nyingine zozote zinahusu usimamizi na hifadhi ya mazingira ambazo idara
itakuwa imepangiwa.
Sehemu katika Idara:
Pamoja na kwamba Idara ina mtaalam mmoja, lakini Idara hii inategemea kuwa na vitengo vitatu kama ifuatavyo:
Huduma zinazotolewa na Idara:
Sheria za mazingira:
Halmashauri ya wilaya inasimamia sheria Na. 20 ya Mwaka 2004 ya usimamizi wa Mazingira. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeunda sheria ndogo ya usimamizi wa Mazingira; sheria hii iliundwa Mwaka 2008.
Sheria ndogo hii ina vipengele kama ifuatavyo:
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.