MAJUKUMU YA KITENGO CHA MICHEZO, UTAMADUNI NA SANAA
Kutoa utaalamu juu ya sanaa, maendeleo ya michezo na kuhifadhi utamaduni. Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:-
(i)Kufanya msako wa utambuzi, maendeleo na malezi ya watu wenye vipaji ili kuongeza ushiriki na ubora katika michezo, utamaduni na sanaa;
(ii)Kuunda na kuratibu uhusiano kati ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, wadau wakuu na wakala kwa ajili ya kukuza utamaduni wa ndani, sanaa na shughuli za michezo;
(iii)(iii) Kuandaa, kuendeleza na kutoa aina mbalimbali za shughuli za kimichezo jumuishi;
(iv)(iv) Kuratibu uhifadhi na ulinzi wa mbuga za jamii na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo na burudani;
(v)Kutayarisha na kutoa fursa za ushiriki wa watu wengi katika michezo, utamaduni na sanaa katika masafa ya umri ili kukuza maisha hai na ya kimwili;
(vi)(vi) Kuandaa tamasha za jamii ili kusherehekea uanuwai wa kitamaduni;
(vii)Kukuza ushiriki wa maendeleo na mafunzo ya wadau wote katika ubora na programu endelevu za michezo, utamaduni na sanaa katika Halmashauri;
(viii)(viii) Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya huduma za elimu na mafunzo katika michezo, utamaduni na sanaa; na
(ix)(ix) Kuratibu na kuandaa matukio ya michezo, utamaduni na sanaa ya shule katika Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.