Kitengo cha ukaguzi wa ndani kimeanzishwa chini ya kifungu 45 (1) cha sheria ya fedha ya mamlaka ya Serikali za mitaa Na 13 ya mwaka 1982.Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Kamati ya Ukaguzi.
Kuandaa Mpango kazi wa Ukaguzi wa ndani wa Halmashauri kila Mwaka.
Kufanya ukaguzi kwa Idara na vitengo vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kama ilivyoainishwa katika mpango kazi.
Kutoa ushauri kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuhusu mfumo wa udhibiti wa ndani na ukaguzi wa nje.
Kuandaa taarifa ya kila robo mwaka na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Mkaguzi wa nje,RAS na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa serikali(IAG).
kutoa ushauri pale utakapohitajika na kufanya ukaguzi maalumu kwa maagizo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
Kukagua na kutoa ushauri sahihi ili kuboresha utawala bora wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Kufanya ufuatiliaji na ukaguzi na usimamizi wa fedha zote za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru zinakusanywa na halmashauri kwa kutumia mifumo ya kieletroniki.
Kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha zote za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na kuandaa taarifa kwa Afisa Masuuli.
Kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na mali za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru pamoja na kuhakiki uwepo wa thamani ya fedha.
Kuhakikisha malengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru yanafikiwa na kuwa na uwajibikaji.
Kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za fedha za serikali zinafuatwa kama zilivyo ainishwa kwenye sheria mbalimbali za serikali
Kufanya kazi nyinginezo kwa maagizo ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Public Finance Act no 6 revised 2004 with its regulations.
Public procurement Act 2004 with its regulations 2005.
Public scheme of service.
Public service Act 2002 and its regulation 2003.
IPPF.
LGFA – (Local Government Finances Act)
Local Authorities Financial Memorandum (LAFM) 2009.
Miongozo na Nyaraka zote za serikali.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.