Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Denis Masanja Ametoa wito huo wakati wa ziara ya kikazi katika Kijiji cha Twendembele kilichopo Tarafa ya Matemanga leo, Alhamisi, Septemba 25, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Denis Masanja ametoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na uharibifu wa vyanzo vya maji na miundombinu yake, amesisitiza kuwa serikali haitavumilia vitendo hivyo vinavyoathiri upatikanaji wa huduma muhimu ya maji kwa wananchi. Ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kikazi katika Kijiji cha Twendembele kilichopo Tarafa ya Matemanga leo, Alhamisi, Septemba 25, 2025.
Onyo hilo linakuja kufuatia kukamatwa kwa wananchi watano (5) wa kijiji cha Twendembele wanaoshukiwa kuhusika na vitendo vya uhujumu na uharibifu wa miundombinu ya maji katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Ameagiza mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine.
Katika ziara hiyo, DC Masanja alitoa maagizo kwa watendaji wa serikali, kuanzia ngazi ya vijiji, kuimarisha ulinzi na usimamizi wa maeneo yote yanayotambuliwa kama vyanzo muhimu vya maji. Alisisitiza umuhimu wa kuweka sheria ndogondogo za vijiji na kata zitakazotoa adhabu kali kwa yeyote atakayepatikana akifanya shughuli zozote zinazokwenda kinyume na hifadhi ya vyanzo hivyo
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.