Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru unaendelea leo tarehe 29 Januari, 2026 katika Ukumbi wa Klasta–Mlingoti.

Pichani: Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika Mkutano wa Baraza
Katika mkutano huo, Waheshimiwa Madiwani wanawasilisha na kujadili taarifa za maendeleo kutoka katika Kata zao, zikiainisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ikiwemo elimu, afya, miundombinu, maji, kilimo na ustawi wa jamii. Lengo ni kutathmini hatua zilizofikiwa, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Pichani:Wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani.
Aidha, mkutano huo unatoa fursa kwa Baraza la Madiwani kutoa maelekezo kwa Menejimenti ya Halmashauri kuhusu maeneo yanayohitaji maboresho ya haraka, pamoja na kusisitiza uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi wa Wilaya ya Tunduru.
Mkutano huu ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kisheria ya Baraza la Madiwani katika kusimamia maendeleo na kuhakikisha miradi ya Halmashauri inaleta tija iliyokusudiwa kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.