HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU
KATA YA MBATI
MHE.RAJABU H.MUSA
DIWANI WA KATA
Namba ya Simu ya Mkononi. +255 789633218
TAARIFA YA KATA YA MBATI
1. UTANGULIZI
Kata ya Mbati ipo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Tarafa ya Nalasi umbali wa kilomita 64 kutoka makao makuu ya wilaya ya Tunduru.Kata hii inapakana na kata ya Mbesa upande wa mashariki, upande wa magharibi kata ya Marumba, upande wa kusini kata ya Nalasi mashariki na upande wa kaskazini inapakana na kata ya Kidodoma na Nampungu.
Katika ngazi ya kata kuna viongozi ambao ni Diwani wa kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa vijiji kuna wenyeviti wa vijiji pamoja na maafisa watendaji wa vijiji.
Kata ya Mbati ina jumla ya vijiji 3 ambavyo ni kijiji cha Mbati,kijiji cha Mdabwa na kijiji cha Mpanji, aidha kata hii ina jumla ya vitongoji vipatavyo 17.
Kata hii ina jumla ya watumishi 22 ambao ni; Mtendaji wa Kata1, Watendaji wa Vijiji 1, Elimu 17, Afya 2,Kilimo, Umwagiliaji Na Ushirika 1, Mifugo Na Uvuvi 0, Maliasili 0, Maendeleo ya Jamii Mtumishi 1 ambaye anafanya kazi ndani ya Tarafa yote ya Nalasi.
Kata ya Mbati ina jumla ya wakazi wapatao 9102 kati ya hao wanaume 3536 na wanawake 5566. Makabila yanayopatikana katika Kata ya Mbati ni kabila la wayao ambalo ni kabila mama, pamoja na kabila la Wanindi na Wamakua ambao ni wahamiaji.
Shughuli kubwa za kiuchumi katika kata hii ni pamoja na Kilimo,Ufugaji na Biashara.
Hali ya ulinzi na usalama ndani ya kata ni nzuri kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama wa raia.
Aidha kila kijiji kina kamati ya ulinzi na usalama,sambamba na majukumu mengine kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.
2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINATOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO.
A.ELIMU
Kata ya Mbati ina jumla ya walimu 17, shule za msingi zipo tatu (3)
B.AFYA
kata ya mbati ina zahanati moja tu (1) na watumishi wawili (2). zahanati hiyo inapatikana katika kijiji cha Mbati.Magonjwa yanayosumbua katika kata hii ni pamoja na Malaria.
C.KILIMO NA USHIRIKA
Kata hii ina mtumishi mmoja tu katika idara ya kilimo.asilimia tisini na nane (98) ya wakazi wa kata ya mbati ni wakulima. Mazao yanayopatikana ndani ya kata ni pamoja na zao la mpunga, Korosho kwa mazao ya Biashara.Mazao ya chakula ni pamoja na zao la Mahindi, mihogo na aina mbalimbali za mnogamboga.
Huduma zinazotolewa na wataalam wa kilimo.
D.MIFUGO NA UVUVI
Idara hii haina mtumishi katika kata hii,mara nyingi anatumiwa mtumishi kutoka idara ya kilimo na ushirika kutoa huduma kwenye idara ya Kilimo na Ushirika. kutoa huduma kwenye idara ya mifugo kwa wananchi.
Idadi ya mifugo iliyopo ndani ya kata ni kama ifuatavyo;
Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwawa ya samaki kwa ajili ya ufugaji wa samaki wenye tija, lengo kuboresha sekta ya uvuvi ndani ya Kata.
E.MALIASILI
Idara haina mtumishi katika kata hii badala yake tunategea watumishi toka ngazi ya wilaya.
Vivutio vya Utalii
katika kata ya mbati kuna vifutio vifuatavyo vya utalii ambayo ni mapango ya matambiko ya kabila la wayao ambayo imezungukwa na msitu wa miti ya asili na mapango hayo yapo kwenye bonde liitwalo LIMATANDA.
Hifadhi ya Wanyamapori
kijiji cha Mpanji katika kata ya Mbati ipo kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi ambayo imetengwa kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori. Idara hii imeendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi wa utunzaji wa hifadhi ya wanyapori na misitu kwa ujumla katika vijiji vilivyopakana na hifadhi hizo. pia zimewekwa alama za mipaka (Biacon) kwa ajili ya kuwatambulisha wanaotaka kuvuka mipaka hiyo kwa shughuli binafsi.
vile vile kuna shughuli za ufugaji nyuki ndani ya kata kwa watu binafsi.
Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo.
Idara inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya misitu asili na vyanzo vya maji kwa matumizi endelevu, kuendelea kushauri kutengwa kwa bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika vijiji na kuendelea kuhamasisha ufugaji bora wa nyuki kwa ajili ya kuongeza vipato.
pia kuwashirikisha wananchi katika kulinda wanyamapori ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa punde wanyama waharibifu wanapohatarisha maisha ya watu na mali zao ili kuweza kuwadhibiti.
F.MAENDELEO YA JAMII
Idara hii ina matumishi mmoja tu ambaye anatoa huduma ndani ya Tarafa yote ya Nalasi. Kazi zinazofanywa na idara hii ni kama ifuatavyo;
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.