Katika hatua kubwa ya kuimarisha sekta ya kilimo na kuongeza uzalishaji wa chakula, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeidhinisha kuanza kwa mradi mkubwa wa umwagiliaji katika Kijiji cha Nambarapi, Kata ya Masonya, Wilaya ya Tunduru. Mkandarasi aliyepewa dhamana ya kutekeleza mradi huu ataanza kazi tarehe 29.07.2024, na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18, kufikia tarehe 31 Desemba, 2025.
Makabidhiano ya mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 6,314,477,066.00 baina ya Tume ya Taifa ya umwagiliaji kwa mkandarasi yamefanyika kwa sherehe za hadhara katika kijiji cha Nambarapi, zimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Simon Chacha, ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Labani Thomas akabidhi Gari saba za wagonjwa katika Halmashauri za Mkoani humo, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ilikabidhiwa Gari Mbili za wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaagiza wakuu wa Wilaya na wakurungenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha miradi yote ya elimu inakamilika kabla ya Desemba 30 mwaka huu.
Ametoa agizo hilo wakati anazungumza kwenye majumuisho ya ukaguzi wa miradi katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru baada ya kukagua mradi wa sekondari mpya ya Kata ya Tuwemacho ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 560 kutekeleza mradi huo kupitia programı ya SEQUIP.
Mkuu wa Mkoa pia ameiagiza TAKUKURU kuchukua hatua mara moja kwa Mtendaji yeyote ambaye amesababisha mradi kutolingana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali hivyo kutekelezwa chini ya kiwango
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.