Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe.Denis Masanja ameendelea kuonesha nia ya kutatua na kuondoa migogoro iliyopo kati ya wakulima na wafugaji, na migongano baina ya binadamu na wanyama,leo tarehe 11.08.2025, amekabidhi mpango wa matumizi ya ardhi kwa Kijiji cha Ngapa. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha ardhi inatumiwa kwa njia endelevu na inayokuza maendeleo.

Mpango huu una lengo la kuweka mipaka wazi ya maeneo mbalimbali, ikiwemo yale ya makazi, kilimo, ufugaji, na hifadhi ya misitu. Unatarajiwa kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara, na pia kuongeza uzalishaji kwa wakulima na wafugaji
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ngapa, Mhe. Masanja alisisitiza umuhimu wa mpango huo katika kuepusha migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikisumbua jamii nyingi. "Mpango huu ni mwongozo wetu. Sasa kila mmoja wetu atajua mipaka ya shamba lake, eneo la malisho, na eneo la makazi," alisema Mhe. Mtatiro. "Tunatarajia kuona maendeleo makubwa yakifanyika katika kijiji hiki kwa sababu sasa tutaweza kupanga shughuli zetu za kiuchumi kwa ufanisi zaidi."
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.