Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Denis Masanja, amekabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 574,257,500 kwa vikundi 227 Hafla ya makabidhiano ilifanyika leo, Agosti 11, 2025, katika ukumbi wa Skyway, ambapo Mheshimiwa Masanja alikabidhi mfano wa hundi kwa vikundi mbalimbali vilivyonufaika.
Mikopo hiyo imelenga makundi yenye mahitaji maalum ya kiuchumi. Kwa ujumla, vikundi 50 vya wajasiriamali wadogo vimenufaika na fedha hizi. Vikundi hivyo vimegawanyika katika makundi makuu matatu: vikundi 24 vya wanawake, vikundi 21 vya vijana, na vikundi 5 vya watu wenye ulemavu. Jumla ya wanufaika ni 227.

Fedha hizi zimekusudiwa kusaidia wanufaika kuanzisha au kupanua miradi yao ya biashara. Lengo kuu la serikali ya wilaya ni kuwajengea uwezo wananchi wake kiuchumi, kuwahamasisha kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali, na hatimaye kuinua maisha yao. Mkuu wa Wilaya aliwakumbusha wanufaika umuhimu wa kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyopangwa ili iweze kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii yao, na pia kurejesha kwa wakati mikopo hiyo.
Aidha, Mikopo hii ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kupitia fedha za mapato ya ndani inaendelea kutolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, na sasa ni dirisha la III, ambapo wananchi wameendelea kuonesha uelewa mkubwa wa kanuni mpya iliyoboreshwa ya utengaji, utoaji na usimamizi wa mikopo 10% ya mwaka 2024, vikundi vyote vilivyokopeshwa katika kanuni hii mpya vimekuwa vikifanya marejesho vizuri kulinagana na makubaliano/mikataba iliyowekwa baina ya halmashauri na kikundi.
Pamoja na changamoto ya ushiriki mdogo wa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kwenye mikutano ya hadhara, wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya wamejitahidi kutoa elimu na semina mbalimbali. Mafunzo hayo yamewapa wanavikundi ujuzi muhimu kuhusu utunzaji wa fedha, uwekaji wa kumbukumbu za biashara, na uwekaji wa akiba.

Kutokana na mikopo hii na mafunzo yanayoambatana nayo, wananchi wa Tunduru wameendelea kukuza biashara zao na kufikia malengo yao ya kiuchumi. Hili ni jambo la kujivunia na linaonyesha ufanisi wa mikopo hii kama chachu ya maendeleo endelevu katika wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.