• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Video

  • TUMEFIKIA asilimia 93 ya makusanyo mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

    August 30th, 2023

    Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imefanya mkutano maalumu wa  kufunga hesabu za fedha kwa mwaka 2022/2023, kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa inayozitaka Halmashauri nchini kufunga hesabu na kuwasilisha kwa mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).

    Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mh. Hairu Mussa alisema, Halmashauri ilikusanya kutoka vyanzo vyake (own source) zaidi ya shilingi bilioni 4.3 ambayo ni sawa na asilimia 93 ya makisio ya mwaka shilingi bilioni 4.7.

    Kutokana na utekelezaji mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo, rasilimali za muda mrefu na mfupi za Halmashauri zimepanda thamani toka zaidi ya shilingi milioni 65 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia zaidi ya shilingi milioni 70 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

    “Mapato tunayokusanya tunahakikisha ,yanaenda katika atekelezaji wa miradi ya maendeleo  katika maeneo yetu ya  kata na vijiji kuboresha huduma za jamii”

    Akifafanua taarifa hiyo, ndugu Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Tunduru ndugu  Masanja Kengese, amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha fedha  shilingi bilioni 4.8.

    “Rai yangu kwa waheshimiwa madiwani kuweza kushirikiana na halmashauri katika kudhibiti mapato, ukizingatia mapato ya halmashauri ya wilaya ya Tunduru yanapatikana kupitia mazao, hivyo, tunawaomba waheshimiwa madiwani kusaidia kudhibiti utoroshaji wa mazao”.

     Alisema.Wakizungumza kwa nyakati tofauti waheshimiwa madiwani  Said Kiosa(kata ya Nanjoka) na Daudi Amlima (kata ya Nakayaya)  wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya  Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Wilaya ya Tunduru.

    Halmahauri ya wilaya ya Tunduru ina Tarafa 7 ,kata 39 ,vijiji 157 na vitongoji 1179 ,Serikali ya Halmashauri  ya wilaya ya Tunduru inahakikisha  maeneo yote yanafikiwa na huduma  za jamii kupitia mapato ya ndani na mapato kutoka Serikali kuu.

  • TUMEFIKIA asilimia 93 ya makusanyo mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

    August 30th, 2023
  • ZAIDI ya kilo milioni 1 za mbaazi kuuzwa Tunduru.

    August 25th, 2023

    Wakulima wa mbaazi wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wamepata dhamana ya kuuza mbaazi kilo1,223,665, zenye thamani Zaidi ya bilioni 2.5 katika mnada wa pili wa mbaazi msimu wa 2023/2024.

    Operesheni meneja Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU LTD), Ndg. Marcelino Mrope amesema kwamba, tani 839 zenye thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilikusanywa katika mnada wa kwanza wa mbaazi kwa msimu huu. Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa uuzaji wa mbaazi katika mnada wa pili Kijiji cha Msinji.

    “Tulifanikiwa kukusanya tani 839 katika mnada wa kwanza wa mbaazi kwa msimu huu na kuuza mbaazi zetu kwa bei ya wastani shilingi 2,016 na kufanya zaidi ya shilingi bilioni 1.6 kuingia katika mzunguko wilaya ya tunduru”. Alisema

    Katika mnada wa pili msimu huu wa mbaazi wanunuzi 15 wamejitokeza kuweka zabuni kununua mbaazi kilo 1,223,665, ambapo wanunuzi watano walifanikiwa kununua mbaazi zote zilizopo ghalani kwa bei ya juu shilingi 2,085 na bei ya chini shilingi 2,075 na kufanya bei wastani kuwa 2,079, ambapo jumla ya shilingi bilioni 2.5 zimeingia katika mzunguko wilaya ya Tunduru. Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU LTD) Ndg. Mussa Manjaule wakati akitangaza bei ya mbaazi katika mnada wa pili wa mbaazi.

    Aidha Ndg manjaule amewasihi wakulima wilaya ya Tunduru kuwa fedha hizi wanazozipata waendelee kuwekeza katika sekta ya kilimo kwa kuwa kilimo ni muhimili muhimu wa uchumi katika wilaya yetu ya Tunduru na kuwaomba kuendelea  kulima Zaidi mazao hayo mbadala ya uchumi.

    “Fedha tunazozipata  tukawekeze, sisi kama wakulima ili tufikie lengo la kupandisha uchumi wa wilaya yetu”

    Mnada wa tatu wa zao la mbaazi katika wilaya ya Tunduru  unatarajiwa kufanyika  mnamo  Agosti 31,2023 katika Kijiji cha Angali .

    Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.

  • ← Prev
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • Next →

Matangazo

  • No records found
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • BENKI ya CRDB yagawa viti na meza 40 kwa Shule ya Sekondari Kungu.

    August 21, 2024
  • WAKAZI wawili wa Tunduru wajishindia zawadi ya Pikipiki na Baiskeli toka kampuni ya TIGO

    August 20, 2024
  • MKUU wa Mkoa wa ruvuma Mhe. Kanali Ahmed A. Ahmed asikiliza kero wananchi wa Tunduru.

    August 20, 2024
  • WAJUMBE wa ALAT Mkoa wa Ruvuma wazisisitiza Halmashauri kusimamia ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

    August 19, 2024
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

Tovuti linganifu

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.