Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Denis Masanja, amewataka wananchikuendelea kushirikiana na serikali ili kudumisha amani ya nchi. Akisisitizaumuhimu wa amani kuelekea kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29Oktoba 2025, kama ilivyotangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, MheshimiwaMasanja, ametoa rai kuwa asitokee yoyote kuwashawishi kujihusisha na vitendoviovu vitakavyofanya kuondoka kwa amani katika nchi yetu. Kauli yake inalengakuhamasisha wananchi kuwa makini na kuepuka vitendo vyovyote vinavyowezakuvuruga utulivu wa taifa, hasa katika kipindi hiki muhimu cha kuelekeauchaguzi.
Akizungumza katika ziara yake katika Tarafa ya Nampungu, Mheshimiwa Masanjaaliendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi kuitunza miundombinu yoteinayotekelezwa katika maeneo yao. Alisisitiza kuwa, waendelee kuitunzamiundombinu yote inayotekelezwa katika maeneo yote ili iweze kuwanufaisha sasana hata vizazi vijavyo, pia, kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inayoanzishwana serikali inatunzwa vizuri na inanufaisha jamii kwa muda mrefu.
Aidha, Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi kuheshimu mpango wa matumizi boraya ardhi. Alifafanua kuwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za kilimohayapaswi kutumika kwa ajili ya shughuli za ufugaji, vivyo hivyo na maeneoyaliyotengwa kwa ajili ya ufugaji. Alitoa maelekezo kwa wafugaji wote kufikakatika ofisi za kijiji, kata, au ofisi za kilimo zilizopo katika Halmashauri yaWilaya ya Tunduru ili kupatiwa maelekezo sahihi kuhusu maeneo yaliyotengwa kwaajili ya ufugaji.
Kuhusiana na suala la ufugaji, Mheshimiwa Masanja ambalo limekua ni moja yaajenda yake kuu katika ziara yake, ameendelea kuwataka wafugaji wote kufikakatika ofisi za kijiji, kata au katika ofisi za kilimo zilizopo katikaHalmashauri ya Wilaya ya Tunduru. Hatua hii inalenga kuratibu shughuli zaufugaji na kuhakikisha wafugaji wanatumia maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao,hivyo kuepusha uvamizi wa maeneo ya kilimo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.