• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

Imewekwa : May 7th, 2025

Mji wa Tunduru umeandika historia mpya katika juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa majisafi kwa wakazi wake kufuatia hafla ya kihistoria ya utiaji saini mkataba wa mradi kabambe. Mradi huu wenye thamani kubwa ya zaidi ya shilingi bilioni 3.2 unalenga kuleta mageuzi makubwa katika huduma ya maji na kukomesha tatizo la uhaba kwa muda mrefu.

Hafla hiyo muhimu iliyoshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Simon Chacha na viongozi mbalimbali wa serikali, uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tunduru (TUUWASA), inatoa matumaini kwa wananchi wa Tunduru kuwa sasa wanaelekea kwenye uhakika wa maji kwa kipindi cha takriban miongo miwili ijayo. Utiaji saini huu unaashiria mwanzo wa safari itakayoboresha maisha ya maelfu ya watu na kuchochea maendeleo endelevu katika wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Simon Chacha, alieleza kuwa mradi huu ni kielelezo cha dhamira ya serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na endelevu ya majisafi. Alisisitiza kuwa upatikanaji wa maji ni msingi muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Vilevile alizisisitiza kampuni hizo zilizotia saini ya kutekeleza mradi huo juu ya kuhakikisha unakamilika kwa muda na viwango vilivyokusudiwa na Wizara ya Maji.

"Utiaji saini wa mkataba huu ni hatua kubwa sana kwa wananchi wa Tunduru," alizungumza Mhe. Chacha "Mradi huu wa Zaidi ya bilioni 3.2 siyo tu utaongeza upatikanaji wa maji, bali pia utaboresha miundombinu yote ya usambazaji, kuhakikisha maji safi na salama yanawafikia wananchi kwa uhakika kwa miaka mingi ijayo."

Mkurugenzi wa TUUWASA Mhandisi.Cuthbert Richard Kiwia alielezea kwa kina kuhusu mradi huo, akifafanua kuwa utahusisha ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa Lita milioni 1, tenki la kwenda juu lenye urefu wa mita 6, ununuzi na uongezaji wa mabomba, ujenzi wa tegeo la maji kwenye mto Nanjoka, ununuzi na ufangaji wa pampu 7, ununuzi wa gari, ujenzi wa kisima cha pampu, ujenzi wa ofisi pamoja na ununuzi wa thamani zake. Mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 3,261,177,554.26 bila ongezeko la kodi.

“Mradi huu utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita millioni 8,283,224, kutoka lita milioni 3.7 ambayo inazalishwa kwa sasa, huduma ya maji itaongezeka kutoka asilimia 78 hadi 100, Zaidi ya wananchi wapatao elf 60 watanufaika, vijiji 20 vitanufaika na mradi huu moja kwa moja, vijiji hivyo ikiwa ni Ujenzi, Exitended, Kalonga, Nakayaya Mashariki, Tuleane, Mkwanda, Majengo, Kalanje, TANESCO, Biasi, Kalonga, Mkwanda, Lambai, Masonya, Ngalinje, Mchangani, Muungano, Nanjoka, National House”. Alibainisha Mhandisi. Kiwia

Mhandisi.Cuthbert Richard Kiwia aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa ili mradi huu ukamilike kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa, kazi hizo ziligawanywa katika kampuni tatu tofauti, ambapo, zabuni ilitangazwa kupitia mfumo wa manunuzi wa serikali (Nest), kampuni hizo zilizoshinda na kupitishwa na bodi ya wazabuni alizitaja kuwa ni one nagg group limited ambaye amesaini mkataba wa shilingi Bilioni 2.1, AKWIJA multake Limited amesaini mkataba wa Milioni 147, Plasco Limited billioni 1.1.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Chacha alimpongeza pia Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Tunduru (TUUWASA) Mhandisi.Cuthbert Richard Kiwia  kwa kazi nzuri anayoifanya, akibainisha kuwa hakujakuwa na malalamiko yoyote hadi sasa, na mipango mipya kabambe ya kuboresha huduma inaendelea kuandaliwa kwa manufaa ya wananchi.

Inatarajiwa kuwa utekelezaji wa mradi huu utaanza hivi karibuni, na utakapokamilika, utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa Tunduru kwa kuhakikisha upatikanaji wa majisafi kwa matumizi ya nyumbani, biashara, na shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi kwa zaidi ya miongo miwili ijayo.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.