• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Video

  • KUELEKEA Mnada wa Mwisho wa Mbaazi Tunduru.

    September 26th, 2023

    Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru ( TAMCU) Kinatarajia kufanya Mnada wa Mwisho wa Mbaazi kwa msimu wa 2023 utafanyika Tarehe 28.09.2023.

    Mnada huo ni fursa muhimu kwa wakulima wa Mbaazi kuuza mazao yao kwa bei nzuri. Wakazi wa Tunduru wanahamasishwa kuhudhuria mnada huo.

    Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu Kitengo cha  Mawasiliano serikalini Wilaya ya Tunduru. 

  • STAKABADHI ghalani ni Mkombozi kwa Mkulima.

    September 13th, 2023

    Mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima na wadau wa masoko ya mazao. Mfumo huu umesaidia kujenga uhusiano mzuri na wa haki kati ya mkulima na mnunuzi wa mazao. Kabla ya mfumo huu, kulikuwa na unyonyaji ambapo wakulima walikuwa wanauza mazao yao kwa bei ya chini sana.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitoa kauli hii katika mkutano wa jukwaa la mifumo ya chakula Africa (AGRF 2023). Alisisitiza kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani umekuwa kiunganishi kizuri baina ya wakulima na soko, na umesaidia kuondoa unyonyaji uliokuwepo hapo awali.

    Mfumo huu umewaletea manufaa makubwa wakulima, hasa katika Wilaya ya Tunduru. Kwa msimu huu, mkulima wa ufuta ameweza kuuza kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kwa kilo moja, na mkulima wa mbaazi ameweza kuuza si chini ya shilingi 1,500 kwa kilo moja. Hii ni bei nzuri na inawawezesha wakulima kupata faida kubwa zaidi.

    Serikali chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe, Dkt.Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za kuboresha miundombinu na mifumo ya kuwezesha mfumo huu wa stakabadhi ghalani. Hatua hizi ni muhimu ili kuhakikisha kuwa kuna muunganiko mzuri baina ya mkulima na mnunuzi wa mazao. Hatua hizi zitawasaidia wakulima kupata masoko bora zaidi na kuondokana na unyonyaji.

    Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa Wilaya zinazoongoza katika kilimo cha zao la Korosho,Ufuta na Mbaazi. Jitihada zake za kuboresha kilimo, kutoa Elimu kwa wakulima, kuimarisha masoko ya ndani na nje zimeleta mafanikio makubwa na kuleta maendeleo ya kiuchumi.

  • TUME kulinda Rasilimali ya Ardhi ya Tunduru.

    September 5th, 2023

    TUME ya Taifa ya Mpango wa matumizi bora ya ardhi (National Land Use Planning Commisio-NLUPC) imeendesha zoezi la kupendekeza, kutathmini na upimaji wa ardhi kwa matumizi mbalimbali katika Wilaya ya Tunduru.

    Mpango huu wa Tume umepitia katika vijiji nane katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambavyo ni kijiji cha Muhuwesi, Liwangula, Ngapa,Chawisi, Mnazi mmoja,Matemanga,Ligunga na Jaribuni.

    Lengo la zoezi hilo ni kuboresha matumizi ya ardhi nchini kwa kuweka mpango madhubuti unaolinda na kusimamia rasilimali ardhi kwa ajili ya matumizi endelevu. Zoezi hili litasaidia kukabiliana na migogoro ya ardhi baina ya watumiaji mbalimbali, vile vile kuwezesha upatikanaji wa Ardhi kwaajili ya uwekezaji katika maeneo hayo.

    Akizungumza Bi Pili Msati ,Msimamizi wa kanda nyanda za juu Kusini -(NLUPC), alisema , lengo la Serikali ni kujenga uelewa kwa wananchi wa maeneo ambayo yana muingiliano wa matumizi ya ardhi ,ili kuweka matumizi bora na sahihi ya ardhi kwa watumiaji tofauti.

    "Tume imekuja kuwezesha mipango kwa lengo la kuweka sawa wastani wa matumizi ya ardhi,lazima tuhakikishe kwamba wananchi wanaishi kwa kuheshimu hifadhi na sehemu zote za ardhi zilizotengwa kwa matumizi maalumu”. Alisema.

    Aidha Mpima Ardhi (W) Tunduru Ndg. Jeremia Nhambu, ameishukuru Serikali kwa kuleta mpango huu, kwani litasaidia kukabiliana na migogoro ya matumizi ya ardhi baina ya watumiaji mbalimbali hasa ya wafugaji na wakulima kwa njia ya Amani na haki. Pia, ameongezea kwa kuwakaribisha wawekezaji kwani mpango huu unaainisha maeneo ya uwekezaji katika maeneo yaliyoainishwa.

    Pia kwa upande wao wananchi wa vijiji vilivyopitiwa na mpango huo ,wameishukuru Serikali kwa mpango huo kwani utapunguza migongano  kati ya wakulima na wafugaji, pia wamehaidi kulinda na kufuata mpango huo wa  Matumizi Bora ya Ardhi.

    Mpango mzuri wa matumizi ya ardhi unaweza kuvutia wawekezaji kwa kutoa mwongozo wa maendeleo ya muda mrefu. Hii inawahakikishia wawekezaji kuwa siasa ya ardhi za eneo hilo ni thabiti na ina misingi ya kisheria, ambayo inaongeza Imani yao katika uwekezaji.

    Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.

  • ← Prev
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • Next →

Matangazo

  • No records found
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MHESHIMIWA,Mhandisi Kundo Aweka Jiwe la Msingi kwa Mradi wa Maji wa Bilioni 3 Tunduru.

    December 13, 2024
  • WAHUDUMU WA AFYA WAPATIWA MAFUNZO YA LISHE WILAYANI TUNDURU

    November 09, 2024
  • MSIBWETEKE KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHAJI LENGO NIKUFIKIA 100%

    October 20, 2024
  • WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WAPATA MAFUNZO YA UCHAGUZI WILAYANI TUNDURU

    October 01, 2024
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

Tovuti linganifu

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.