Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Denis Masanja alitoa agizo kali kwawale wote waliohusika katika kuuza mashamba kiholela kwa wafugaji. Aliagiza,"Wale wote waliohusika katika kuuza mashamba kiholela kwa wafugajiwarejeshe fedha hizo, na wafugaji hao waondoke kwa hiari haraka iwezekanavyokuelekea katika maeneo yaliyotengwa (vitalu) kwa ajili ya shughuli zaufugaji."
Zoezi la kuwabaini na kuwaondoa wafugaji wote kwenye maeneo ya wakulima kwahiari limeanza toka tarehe 21 Julai 2025 na litahitimishwa tarehe 15 Agosti2025. Baada ya hapo, Mheshimiwa Masanja Alimalizia kwa onyo kali, kwamba, baadaya hapo wafugaji wote waliopo kwenye maeneo ya wakulima wataondoshwa kwa nguvu,iwapo hawatatii agizo hilo la kuondoka kwa hiari.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.