• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

NANDEMBO YAUNGANA KWA AMANI: WANANCHI WAPATIWA ELIMU YA UPENDO NA MSHIKANO KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII

Imewekwa : February 8th, 2026

Wananchi wa Nandembo wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu wa Amani, Upendo na Mshikamano katika kushiriki na kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwa ni pamoja na misiba, harusi na michezo, ili kuimarisha mahusiano mema na mshikamano ndani ya jamii.


Elimu hiyo ilitolewa na viongozi wa Jukwaa la Viongozi wa Dini Wilaya ya Tunduru, wakiongozwa na Mchungaji Emmanuel Kanduru, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, pamoja na Shekhe Zuberi Mnandi, Katibu wa Jukwaa la Viongozi wa Dini Tunduru. Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa ushirikiano miongoni mwa wanajamii bila kujali tofauti za kidini, wakieleza kuwa amani na mshikamano ni msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Aidha, sambamba na utoaji wa elimu hiyo, wananchi wa Nandembo walipata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu (draft) na mchezo wa bao, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kuleta jamii pamoja katika mazingira ya amani na furaha.


Kupitia udhamini wa Shirika la FPCT-STCC, linalotekeleza Mradi wa Kuimarisha Amani, Upendo na Mshikamano kwa waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini, washindi wa michezo hiyo walipatiwa zawadi. Mshindi wa mchezo wa mpira wa miguu alipatiwa jezi, huku mshindi wa pili akipatiwa mpira, ili kuendelea kuendeleza shughuli zao za kimichezo.

Tukio hili limeonesha kwa vitendo namna Serikali, taasisi za kidini na vikundi vya wanajamii, ikiwemo timu za michezo, vinavyoweza kushirikiana katika kuleta wananchi pamoja, kutoa elimu kwa jamii na kuchochea mabadiliko chanya yanayojenga mshikamano na amani ya kudumu katika jamii.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • NANDEMBO YAUNGANA KWA AMANI: WANANCHI WAPATIWA ELIMU YA UPENDO NA MSHIKANO KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII

    February 08, 2026
  • MAFUNZO YA MFUMO WA NEST YAWAWEZESHA MAFUNDI WA NDANI, MAKUNDI MAALUM NA WAZABUNI KUSHIRIKI ZABUNI ZA SERIKALI.

    February 07, 2026
  • FURSA NA ELIMU YA KODI ZAWAFIKIA LOCAL FUNDI, MAKUNDI MAALUM NA WAZABUNI TUNDURU.

    February 07, 2026
  • ELIMU YA FURSA ZA KIUCHUMI ZAWAFIKIA VIJANA WA BODABODA, BAJAJI NA MAGUTA TUNDURU.

    February 07, 2026
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.