Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeendesha mafunzo maalum kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika ngazi ya kata katika jimbo la Tunduru Kusini na Kaskazini, Mafunzo hayo yataanza leo tarehe 4 hadi 6 mwezi Agosti, 2025. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wa kusimamia uchaguzi kwa weledi, uadilifu, na kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wameapa kutunza siri zote za shughuli za uchaguzi. Kiapo hiki kinawalazimu kutofichua au kutoa taarifa za siri za uchaguzi kwa mtu yeyote asiyehusika. Hii inalenga kuhakikisha uadilifu wa mchakato mzima wa uchaguzi na kuzuia upotoshaji wa taarifa. Kwa mfano, wameapa kutotoa taarifa za matokeo ya kura kabla ya kutangazwa rasmi na mamlaka husika.
Pamoja na kiapo cha kutunza siri, wasimamizi hawa wametoa tamko rasmi la kujitoa kwenye vyama vya siasa. Hii ni hatua muhimu ya kuhakikisha wasimamizi hawa wanatekeleza majukumu yao kwa haki na usawa bila upendeleo wa kisiasa. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesisitiza kuwa msimamizi wa uchaguzi anatakiwa kuwa huru na kutopendelea upande wowote ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, uadilifu na uhuru.

Mafunzo haya yanaashiria maandalizi makubwa ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya kuelekea uchaguzi wamwaka 2025, huku ikihakikisha wasimamizi wanakuwa na utayari wa kutosha kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi kwa ufanisi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.