Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inajiandaa kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa, unaotarajiwa kugharimu shilingi bilioni 1.4, fedha zitakazotokana na mapato ya ndani ya halmashauri. Katika hatua ya kuhakikisha ufanisi na usimamizi bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndugu Chiza Marando, ameunda Kamati Maalum ya Ujenzi. Kamati hii ina jukumu muhimu la kusimamia mradi huu tangu mwanzo hadi mwisho, ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika.

Mkurugenzi Mtendaji Marando, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu na miongozo yote ya manunuzi ili kuhakikisha uwazi na ufanisi katika matumizi ya fedha.
Kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa, kazi za ujenzi wa ukumbi huu zinatarajiwa kuanza kabla ya tarehe 15 Agosti, 2025. Maandalizi yote yanaendelea kufanyika ili kuhakikisha mradi huu unaanza kama ilivyopangwa. Kukamilika kwa ukumbi huu kutachangia pakubwa katika maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na kuboresha mazingira ya kazi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.