• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

WAZEE WATAJWA NGUZO YA MAENDELEO: MWENYEKITI HALMASHAURI YA TUNDURU AZUNGUMZA NA WAZEE WA WILAYA.

Imewekwa : February 4th, 2026

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Seif Dauda, leo Jumatano tarehe 4 Februari 2026, ameongoza kikao maalum cha pamoja na wazee wa Wilaya ya Tunduru kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri. Kikao hicho kililenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya wilaya pamoja na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Pichani:Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Mhe. Seif Dauda

Katika kikao hicho, wajumbe walipata fursa ya kujadili kwa kina changamoto zinazowakabili wananchi wa Wilaya ya Tunduru, zikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za afya, umeme, miundombinu ya barabara pamoja na usalama wa raia. 

Mhe.Dauda alisisitiza kuwa wazee ni nguzo muhimu ya maendeleo katika Wilaya ya Tunduru. Alieleza kuwa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya uongozi na wazee kutasaidia kutatua changamoto kwa urahisi na kwa wakati. Hivyo, aliwahimiza wadau wote kuimarisha mshikamano, ushirikiano na mawasiliano ya karibu ili kuhakikisha maendeleo endelevu yanapatikana kwa manufaa ya wananchi wote wa Wilaya ya Tunduru.

Pichani:Baadhi ya Wazee walaya ya Tunduru.

Akitolea ufafanuzi kuhusu changamoto zilizowasilishwa na wazee, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Ndugu Chiza Marando, alieleza kuwa Halmashauri itahakikisha changamoto zote zilizobainishwa zinafanyiwa kazi kwa kushirikiana na taasisi husika. Pia aliahidi kuzingatia na kufanyia kazi ushauri uliotolewa na wazee hao, sambamba na kuendeleza na kudumisha uhusiano mzuri kati ya wazee na uongozi wa Halmashauri.

Aidha, kikao hicho kilijadili mikakati ya kuimarisha ushirikiano kati ya uongozi wa Halmashauri na wazee katika kusimamia, kushauri na kusukuma mbele ajenda za maendeleo na kijamii ndani ya wilaya.


Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • WAZEE WATAJWA NGUZO YA MAENDELEO: MWENYEKITI HALMASHAURI YA TUNDURU AZUNGUMZA NA WAZEE WA WILAYA.

    February 04, 2026
  • HALMASHAURI YA TUNDURU YAWAFIKIA VIJANA BODABODA NA BAJAJI, YAWAFUNGULIA MILANGO YA FURSA ZA KIUCHUMI.

    February 04, 2026
  • TAARIFA KWA UMMA

    February 04, 2026
  • MKURUGENZI MARANDO AAGIZA MIRADI YOTE IKABIDHIWE IFIKAPO TAREHE 01 MACHI, KAZI IFANYIKE USIKU NA MCHANA.

    February 03, 2026
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.