Local Fundi, makundi maalum na wazabuni kutoka Wilaya ya Tunduru wamepatiwa elimu maalum kuhusu makato ya kodi na wajibu wa mlipa kodi, Mafunzo yamefanyika leo ,tarehe 07/02 katika ukumbi wa Klasta-Mlingoti.

Mafunzo haya, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), yalihusisha pia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliokaribishwa kutoa elimu maalum kwa washiriki.
Mwezeshaji kutoka TRA, Bwan.Chiza Linus, Afisa Kodi Msaidizi kutoka Songea, alitoa elimu kwa washiriki kuhusu makato mbalimbali ya kodi zinazohusiana na zabuni, ikiwemo kodi ya zuio (withholding tax), wajibu wa mlipa kodi na umuhimu wa kufuata sheria za mapato.

TRA pia imesisitiza kuwa ni mshirika muhimu wa wafanyabiashara na wazabuni, tayari kutoa ushauri na msaada pale wanapohitaji kufahamu masuala ya kodi. Pia, walieleza kuwa kila Alhamisi ya kila wiki, ofisi za TRA zimepangwa kuwa siku ya kuzungumza na walipa kodi, na washiriki wanashauriwa kufika siku hiyo kuwasilisha changamoto zao.
Aidha, ndg. Hassan Suker, Afisa Kodi kutoka Songea, amewasisitiza washiriki umuhimu wa kutunza risiti zote pamoja na kumbukumbu sahihi za malipo, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuthibitisha miamala ya kifedha, kurahisisha ukaguzi wa kodi, kuepuka migogoro ya kikodi na kulinda haki za wazabuni kwa mujibu wa sheria.

Washiriki wameeleza kuridhishwa na elimu waliyoipata, wakibainisha kuwa itawasaidia kushiriki zabuni za Serikali kwa ufanisi, kuboresha usimamizi wa biashara zao na kujenga uaminifu kwa TRA.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.