Uongozi wa wilaya Tunduru wakifuatilia kwa karibu kabisa Taarifa ya Tathmini ya Elimu wilaya, katika picha ni mkuu wa wilaya Juma Zuberi Homera na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg Chiza C.Marando
Afisa Elimu Taaluma wilaya akisoma taarifa ya mwenendo wa taaluma wilaya ya tunduru kwa mwaka 2017 katika kikao cha tathmini ya elimu wailya kilichofanyika katika ukumbi wa klasta Tunduru
Maafisa Elimu Sekondari na Msingi wilaya ya Tunduru wakifuatilia mjadala katika kikao cha tathimini ya elimu kilichofanyika februari 6 2018
mkuu wa wilaya Tunduru Juma Zuberi Homera akitoa maagizo kwa waratibu Elimu Kata, Watendaji Kata na Watendaji wa vijiji katika kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali, pia kusimamia katika maeneo yao ya kazi na kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanenda shule, na wale wa awali na darasa la kwanza waliosajiliwa wanaripoti shuleni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg.Chiza C.Marando akitoa maelekezo kwa wakuu wa shule za msingi na sekondari kushirikiana na watendaji kata na vijiji katika maeneo yao ya kiutendaji na kubainisha mahitaji katika shule zao ili waweze kupatiwa fedha za kuboresha miundombinu ya elimu kupitia fedha za mfuko wa Elimu wilayani
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Tunduru Mh.Mbwana Mkwanda Sudi akitoa mbinu za kuongeza kiwango cha ufaulu wilyani Tunduru na kuondoa kinyago kabisa wakati wa kikao cha Tathimini ya elimu wilaya
wadau wa Elimu wilaya ya Tunduru wakiwa katika kikao cha tathimini ya elimu wilaya katika kufanya maboresho katika sekta ya elimu
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.