Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Tunduru, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Simon Kemori Chacha, pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya, wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru 2024.
Katika ziara hiyo, Mhe. Chacha alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi, wananchi na wadau mbalimbali katika kukamilisha miradi hii kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa. Aliagiza wasimamizi wa miradi kuhakikisha inasimamiwa kwa ukamilifu na kwa uwazi ili kukidhi matarajio ya wananchi.
Ziara hii ni sehemu ya maandalizi ya kina yanayofanywa na Wilaya ya Tunduru kuhakikisha maadhimisho ya Mwenge wa Uhuru 2024 yanafanikiwa na yanaleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa katika kijiji cha Sauti Moja tarehe 8 Juni 2024. Ambapo, Mhe. Chacha aliwahimiza wananchi wote kujitokeza kwa wingi kupokea mwenge huo, ambao ni alama ya uzalendo na umoja wa taifa.
Miongoni mwa miradi iliyopitiwa na kamati ni pamoja na Ujenzi wa madarasa matatu mapya ,kiwanda cha kuongeza thanani mazao ya misitu, jengo la EMD ,Madarasa mawili ya TEHAMA KIUMA pamoja na shughuli za kilimo KIUMA ,Mradi wa maji safi na salama.
Mhe. Chacha ameeleza kuridhika kwake na maendeleo ya miradi hii na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa watekelezaji ili kukamilisha miradi hii kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.