Maadhimisho ya Siku ya Familia Yafanyika Kata ya Namasakata, Tunduru
Maadhimisho Siku ya Familia Duniani hufanyika kila mwaka Mei 15, katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru maadhimisho hayo yatafanyika Kata ya Namasakata.
Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo, Bi. Getruda Ngole, ameeleza kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuthamini mchango wa familia katika ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Bi. Ngole ameongeza kuwa Siku ya Familia Duniani ilianzishwa mwaka 1993 na Umoja wa Mataifa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa familia,
“Familia ni msingi wa jamii bora na ndio chimbuko la maadili mema na malezi bora kwa watoto”.Alisema Bi Ngole
Afisa Ustawi wa Jamii, Ndg. Nelson Yohane, amesisitiza umuhimu wa malezi bora kwa watoto katika kujenga familia bora. Alisema kuwa mfumo bora wa malezi unaanza katika familia na unaendelezwa katika jamii na taasisi za kidini.
Maadhimisho ya Siku ya Familia yatajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo michezo ya watoto, burudani, na utoaji wa mahitaji maalumu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Diwani wa Kata ya Namasakata, Mheshimiwa Mussa Husanje.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inaomba wananchi wote kushiriki katika maadhimisho haya ili kuonyesha umuhimu wa familia katika jamii yetu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.