Mbunge wa jimbo la Tunduru Kusini Mhe. Idd D. Mpakate, Diwani wa Mbati Mhe. Tayson, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndg. Chiza C. Marando aliambatana na timu ya wataalamu kutoka idara ya ujenzi, elimu sekondari na Mipango kwenda kukagua na kujiridhisha eneo lililotengwa pamoja na nguvu za wananchi zilizoanza kufanya shughuli za ujenzi wa shule tarajali katika kata ya Mbati
Ziara hiyo ya Jumamosi tarehe 13.7.2024 Mhe. Mpakate alitumia nafasi hiyo kuwaelezea wananchi namna serikali inayoongozwa na Daktari Samia Suluhu Hassani inavyowathamini wananchi wa Mbati na awamu hii imewapatia fedha kiasi cha shilingi 560,552,827 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari katika kata ya Mbati kitu ambacho wamekuwa wakiomba kwa muda mrefu.
Pichani ni Wananchi wa Kata ya Mbati wakiwa katika mkutano.
Diwani wa kata ya Mbati Mhe. Taisoni pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbati walimshukuru Mhe. Rais kwa kuwaletea fedha hizo, Mhe Mbunge kwa mapambano yake kuhakikisha anapata gawio kwa ajili ya wananchi wa Mbati. Walisisitiza kuwa hakuna shaka mradi huo utatekelezwa kwa wakati kadri ya maelekezo ya serikali.
Pichani ni Diwani wa kata ya Mbati Mhe. Taisoni
Aidha, Ndg. Marando alieleza kuwa atahakikisha kuwa anasimamia mradi huo usiku na mchana huku akisisitiza juu ya uwajibikaji wa kila mwananchi, kulinda na kutunza mali na vifaa vya ujenzi muda wote na hatofumbia macho wizi, upotefu au ubadhilifu wa aina yeyote ili ukamilike kwa wakati na ifikapo January 2025 wanafunzi waanze kusoma.
Kwa upande wake Mhandisi wa Halmashauri Eng. Ramadhani Magaila alitoa ufafanuzi wa namna jengo litavyokuwa kama maelekezo ya serikali yanavyosema, pia aliwaomba wananchi kushiriki vizuri hasa kwenye maeneo yanayohitaji nguvu za wananchi (20%) kama shughuli za kusafisha eneo, kuchimba msingi, kifusi pamoja na maji.
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Mwl. Mussa Chandu aliwaomba wana Mbati kupokea kwa mikono miwili mradi huo kwa kuhakikisha wanaungana kuukamilisha kwa wakati na ifikapo January watoto waanze masomo huku akiwasisitiza umuhimu wa kuwapeleka watoto shule na kuwasimamia wamalize tofauti na hapo awali ambapo shule ilikuwa mbali.
Wananchi wa kata ya Mbati walimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anawatengenezea miundombinu ambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma ya Elimu kwa watoto wao.
Imetolewa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru,
Orpa Kijanda,
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.