Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh. Wakili Julius S. Mtatiro ameendelea kukagua miradi ya maendeleo katika Shule za Sekondari za Tunduru, Mataka, Nandembo na Masonya, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kikazi aliyoianza tarehe 21 .09.2023.
Katika ziara hiyo, Mh. Wakili Mtatiro alikagua Majengo ya Madarasa, Mabweni, na vyoo. Alitoa maagizo kwa viongozi wa Shule na wakandarasi wa miradi hiyo kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, kwani kukamilika kwa majengo hayo kutaboresha mazingira ya kusomea na kufundishia, hivyo kusaidia kuinua kiwango cha Elimu katika Wilaya ya Tunduru.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mh. Wakili Mtatiro alisema kuwa anaridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo kwa ujumla, lakini alielekeza maeneo machache kuboreshwa. Alisisitiza kuwa majengo yote yakamilike kwa ufanisi, ubora na kwa wakati.
“Miundombinu hii ni muhimu katika kuhakikisha Wanafunzi wanapata Elimu Bora, wataalamu wa Shule zote zinazoendelea na miradi mshirikiane katika hatua zote ili kuepuka kurudia makosa” Alisema Mh. Wakili Mtatiro.
Mh. Wakili Mtatiro aliahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassani katika kuboresha miundombinu ya Elimu katika Wilaya ya Tunduru ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata Elimu Bora.
Ziara ya Mkuu wa Wilaya inasaidia kuangalia maendeleo ya Miradi ya maendeleo inayoendelea katika Wilaya ya Tunduru.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.