Katika muendelezo wa Ziara ya kikazi ya mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Tunduru adv. Julius S. Mtatiro katika shule za sekondari wilaya ya Tunduru ,leo mei 16, 2023 ameongea na watumishi walimu katika shule tatu za sekondari tarafa ya lukumbule. Alizungumza na watumishi walimu katika shule ya sekondari semeni,sekondari ya lukumbule na sekondari ya mpakate.
Mkuu wa wilaya alisisitiza katika eneo la ufaulu wa kitaaluma, aliwataka wakuu wa shule za sekondari semeni ,lukumbule na mpakate kuweka mikakati imara ya ndani ya shule ili kuwezesha kupandisha ufaulu ,katika eneo hilo hilo aliwataka wakuu wa shule kujitahidi kuzidi kupunguza au kuondoa kabisa madaraja ya chini ambayo ni daraja la nne na daraja sifuri .
"Watoto hawa wanahitaji kupatiwa msaada wa kiakili na kimaadili kalingana na mazingira yao ya nyumbani"
Aliwataka watumishi walimu kuwa karibu na wananfunzi katika malezi yao ya kijamii ili kuwatengeneza katika hali bora ya kisaikolojia na pia kuwapa huduma za ushauri na unasaha.
Aidha aliwaomba kuwa na ushirikiano,umoja na upendo baina ya watumishi walimu katika shule zote ili kuongeza uwezo wa kujenga na kupandisha ufaulu katika shule zetu za wilaya ya Tunduru.
Aidha kwa msisitizo aliendelea kuutaka uongozi wa kata kushirikiana na uongozi wa shule kusimamia suala zima la chakula kwa wanafunzi kwa kuimiza wazazi na walezi kuendelea kuchangia chakula shuleni.
Mwisho aligusia suala la mahusiano haramu yaliopo baina ya walimu na wanafunzi kwa kuwataka viongozi wa shule kushughulikia hili kwa kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya watumishi walimu kwa ukaribu mkubwa, ili kusiwepo na mahusiano ya aina hiyo katika shule, kwasababu kufanya hivo ni kosa kisheria .
"JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA"
"KAZI IENDELEE"
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.