Katika muendelezo wa ziara ya kikazi ya Balozi wa msumbiji nchini Tanzania Mhe.Ricardo Mtumbwuida katika mkoa wa Ruvuma leo May 24,2023 ametembelea katika wilaya ya Tunduru
Barozi Mhe. Mtumbwuida ametembelea katika moja ya eneo ambalo mashujaa wapigania uhuru wa msumbiji waliweka kambi wakati wa ukombozi wa nchi ya msumbiji na ukoloni,katika matembezi hayo barozi Mtumbwuida alitembelea ukumbi ambao Samora Machel alihutumia kutolea mafunzo ya kijeshi kwa wapiganiaji hao,pia nyumba walizokuwa wakiishi wakati huo wa kambi na pia eneo ambalo mkutano mkuu wa kwanza wa umoja wa wanawake wa chama cha frelimo ulifanyika na sehemu ya maandaki ambapo wapiganaji hao waliyatumia katika kujihifadhi wakati wa mapigano.
Balozi Mtumbwuida alizungumza na wananchi wa msumbiji waliopo katika wilaya ya Tunduru na kuwataka kuzidi kudumishi amani ,uadilifu na upendo walioukuta katika nchi ya Tanzania ili kuendeleza umoja na mshikamano uliopo baina ya nchi hizi mbili, na kuwahaidi kuweza kujitahidi kutatua changamoto zao zinazowakabiri kama wananchi wa msumbiji.
Balozi pia alizungumza na umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kuzidi kuonesha uzalendo katika nchi yao ili kuzidi kulifanya taifa la Tanzania kudumu katika hali ya kimaendeleo na kuzidi kuonesha ushirikiano baina yao na wenzao wa jirani frelimo (msumbiji.)
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.