Akiwa katika ziara ya siku nne ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Jimbo la Tunduru kusini mbunge wa Tunduru kusini Mh. Daimu Mpakate alifanya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba ya mganga katika zahanati ya Naikula, ukarabati wa kisima cha Maji katika cha Mkasale na ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya Mkasale.
Akiwa katika zahanati ya Naikula mbunge wa Tunduru Kusini alisisitiza matumizi ya nguvu za wananchi katika miradi inayopelekwa na serikali ili kuongeza wigo na utoshelevu wa fedha zinazotolewa kukamilisha mradi husika na kwa wakati, kutochangia wananchi kunarudisha nyuma maendeleo na mipango ya serikali katika kuboresha huduma za afya.
Aidha Mh Mpakate alisema serikali ya awamu ya tano ina vipaumbele vyake katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020 ambayo ni kusogeza Huduma za afya kwa wananchi wake, kuboresha Huduma za Elimu na huduma za maji, hivyo ni vizuri kwa diwani ambaye ni msimamizi wa maendeleo kata kusimamia na kuhimiza wananchi kushiriki katika kuchangia miradi inapofika katika maeneo yao ya kiutawala.
Mbunge wa Tunduru Kusini akitoa maekelezo kwa Mhandisi Majenzi wilaya Ndg Kivuyo akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika tarafa ya Namasakata alipofika akufanya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba ya mganga katika zahanati ya Naikula ambao upo katika hatua ya Boma, kulia kuoka kwake ni Kaimu mhandisi majenzi, Mganga mkuu wilaya Dr Wendy Robert, na Afisa Elimu Takwimu, vifaa na vielelezo wilaya mwalimu Shaban Mangosongo.
Alisema katika kijiji cha Mkasale kumekuwa na kisima cha muda mrefu ambacho kimeharibika lakini serikali katika kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani imetenga milioni 13,000,000 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kupitia mfuko wa PBR na mfuko wa kuchochea maendeleo jimbo kwa ajili ya kufanya ukarabati wa miundombinu ya Maji.
Aidha mradi huu wa ukarabati wa maji katika kijiji cha Mkasale unakadiriwa kukamilika baada ya miezi miwili ili kuanza kutoa Huduma kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya upatikanaji maji katika kituo cha afya Mkasale alisema mbunge wa Tunduru kusini.
Vilevile alitembelea katika ujenzi wa kituo cha Mkasale ambapo kunafanyika ujenzi wa wodi ya Mama na Mtoto, Maabara,Nyumba ya Mtumishi, Chumba cha Kuhifadhia Maiti (Mortuary), Chumba Cha Upasuaji (Theatre) Na Kichomea Taka na Placenter Pit ambao unagharimu jumla ya milioni 400 zimetngwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo na milioni 300 ni kwa ajili ya kununua vya kitabibu vitakavyotumika katika kutolea huduma katika kituo hicho baada ya kukamilika.
Jengo la nyumba ya mganga mradi unaotekelezwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018
Akiwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji vya Mkotamo na Mkasale Mbunge wa Tunduru Kusini Mh.Daimu Mpakati alishukuru kwa mradi huu kupelekwa katika kituo cha afya mkasale kwani ni miongoni mwa vituo vya afya 200 vilivyopata mgawo wa fedha lakini pia nchini kuna zaidi ya vituo vya afya 500, hivyo mradi huu ungeweza kupelekwa kwingine lakini serikalini imesikia kilio cha muda mrefu cha wanatunduru.
“Mh Mpakate alisema Tanzania ina zaidi ya vituo vya afya 500 lakini katika hivyo wilaya ya tunduru tumepata mgawo wa shilingi milioni 700 , ambapo milioni 400 zimeelekezwa katika kufanya upanuzi wa majengo ya kituo hiki cha Mkasale na nyingine 300 kwenda kununua vifaa tiba”
Aliendelea kutabaisha kuwa wananchi wanatakiwa kuimiliki mradi huu kwani ni mali yao na kutoa ushirikiano wa karibu ikiwa ni pamoja na kusaidia katika kazi ikiwemo kushusha tofali na kwenda kupakia tofali ili kupunguza gharama zisizo za lazima ambazo wanalipwa vibarua ambafedha hizo zingebaki na kuongeza majengo zaidi katika kituo hicho kwani kwa sasa yatajengwa majengo sita kwa kadiri ya kipaumbele lakini lengo ni kujenga majengo 12.
ukaguzi wa ukarabati wa mradi wa maji katika kijiji cha Mkasale unatarajiwa kutumia milioni 13 hadi kukamilika kutoka katika mfuko wa Jimbo na Mfuko payment for big result (PBR)
Hata hivyo aliwataka wananchi, wazazi, walezi na wananfunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2017 ambao bado hawajaripoti shuleni kufanya hivyo mara moja kwani ufikapo mwezi wa tatu kama kuna mzazi au mlezi yuko namwanafunzi nyumbani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashitaka.
diwani wa kata ya namasakata mh Usanje akitoa changamoto za wananchi kwa Mh.mbunge wa Tunduru kusini juu ya ukosefu wa nguvu kazi ya wamnanchi unaosababishwa na kauli za viongozi wa serikali katika mradi wa ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Mkasale.
Naye mwenyekiti wa CCM wilaya alisema aliwataka wananchi wa tunduru kuacha tabia ya kuwazuia wattoto kwenda shule na kuwataka waige mifano kutoka kwa jamii za mikoa ya kaskazini ambao wamewekeza kwa asilimia kubwa katika elimu na kwa wana maendeleo ukilinganisha na kusini ambapo hawaoni umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.