Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa atafanya ziara ya kikazi mkoani Ruvuma kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 25 katika Wilaya za Namtumbo na Tunduru kukagua shughuli za maendeleo, kuongea na watumishi, kufanya uzinduzi wa ghala na Kukagua Ujenzi wa Kituo cha Afya Nakayaya.
akitoa taarifa ya Ziara iyo wilayani Tunduru Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera amesema moja waziri mkuu atatembelea vijiji vya Mbungulaji na Rahaleo kukagua mradi wa maji na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Rahaleo, na akiwa njiani kuelekea Tunduru atasalimiana na wananchi katika kijiji cha Milonde.
Mkuu wa Wilaya Homera aliendelea kusema kuwa Waziri mkuu atafanya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi, kukagua ujenzi wa ghala la korosho eneo nakayaya, kukagua ghala la Korosho Afrika la kuhifadhia korosho ghafi Tunduru, na kupata Taarifa ya Ununuzi na uuzaji wa Korosho kwa msimu wa mwaka 2017/2018 kutoka kwa chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU).
baada ya ukaguzi huo Waziri Mkuu Mh.Kassimu Majaliwa atapata fursa ya kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wote katika uwanja wa mpira (CCM) kutoa maelekezo ya serikali na kusikiliza kero, Maoni na Changamoto za wananchi wa wilaya ya Tunduru.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera anawaalika wananchi na watumishi wote kufika bila kukosa katika mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 24/11/2017 katika uwanja wa mpira Tunduru Mjini ili kuweza kumsikiliza kiongozi wao kwani muhimu sana kujua amewaletea nini wanatunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.