Zoezi la usainishaji wa mikataba ya utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya Kata na kijiji limenguliwa na mkuu wa wilaya ya tunduru Julius S mtatito, ukiwa na lengo la kuboresha hali ya lishe na kuondoa athari za utapiamlo katika jamii, na kufanya suala la lishe kuwa ajenda kuu ya kudumu katika mabaraza ya maendeleo ya Kata.
Akiongea na watendaji wa Kata wakati wa kusaini mkataba wa utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya Kata mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius S. Mtatiro alisema masuala ya lishe ni mapana sana ambayo yanahusisha sekta mbalimbali kama kilimo, Mifugo, Afya, Maji.
Masuala ya lishe sio jambo la kitabibu pekee ni jambo la kijamii na wilaya imeanza kuchukua hatua ya kutokomeza udumavu, ukondefu, uzito pungufu na upungufu wa vitamin kwenye makundi maalum.
watendaji wa Kata wakifuatilia kwa makini maagizo ya mkuu wa wilaya Julius Mtatiro
Mkuu wa wilaya huyo aliwataka watendaji Kata kutumia nafasi zao katika jamii kuhakikisha suala la lishe linakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vya maendeleo ya Kata, “ninataka watendaji wote wa kata mwende mkatumie nafasi zenu kwa kuwa nyie ndio injini ya utekelezaji wa kazi, nitaanza kukagua mihtasari ya vikao vya mabara ya kata kuona kama suala la lishe limekua ajenda ya kudumu katika vikao vyenu kuona kama lishe imekua ajanda kwenye vikao vitakavyofanyika kanzia sasa” alisema Mkuu wa wilaya Julius Mtatiro.
Aliendelea kutabaisha kuwa lishe ni msingi na uti wa mgongo wa uhai wa mwanadamu na lishe ni kitu ambacho hakikwepeki, kila kata iende kutengeneza mpango kazi wa utekelezaji wa afua za lishe katika Kata na Vijiji na kusimamia.
Akitoa mfano wa aina ya watendaji katika mikoa 12 aliyotembelea mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa serikali ina watendaji Kata wenye ueledi mkubwa sana, zaidi ya asilimia 70 ni wazuri lakini wengi wao wanakwepa kutekeleza majukumu yao kwa visingizio tofauti visivyokua na tija.
Aidha alisema utekelezaji wa afua za lishe unaenda sambamba na usafi wa mazingira, mazingira safi kwa maeneo ya kutoa huduma hasa za chakula, “opesheni ifanye katika maeneo yanayotoa huduma za chakula, kila mtendaji akatoe elimu kwa wananchi kabla ya kuwakata, utolewe muda ili kama hawajatekeleza ndio hatua zifuate.
Hata hivyo alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji kupitia baraza la madiwani kutunga sheria ndogo itakayosimamia utekelezaji wa afua za lishe itakayowabana wananchi, tukitunga sheria ndogo iatasaidia jamii kushiriki moja kwa moja katika kuondoa tatizo la udumavu ndani ya wilaya ya Tunduru.
Naye afisa lishe wilaya Bi Martha Kibona amesema mikata hii hii inalenga katika kuboresha hali ya lishe na kuondo tatizo la udumavu na utapiamlo kwani watendaji wa kata ndio viongozi ambao wataenda kusimamia utelekezaji wa afua za lishe na kufikia malengo yaliyowekwa na serikali kuwa na jamii isiyokuwa na udumavu, uzito pungufu, utapiamlo na ukondefu ifikapo 2021.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.