WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WAPATA MAFUNZO YA UCHAGUZI WILAYANI TUNDURU
Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru,Ndugu Chiza C Marando ameendesha mafunzo ya Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ili kuwapa uelewa mzuri wa kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27 Novemba,2024. Mafunzo haya yamefanyika leo tarehe 30 Septemba , 2024 katika ukumbi wa Klasta.
Lengo kuu la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa Wasimamizi hao wanafahamu sheria za Uchaguzi, kanuni za uendeshaji, na umuhimu wa uwazi na haki katika mchakato mzima.
Msimamizi wa uchaguzi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao, ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki kwa wananchi wote wanao tuzunguka katika maeneo yetu.
Pia Ndugu Chiza Marando amewataka kuyashika na kuyaishi mafunzo hayo kwa sababu ndio muongozo na kanuni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa ili kufanya uchaguzi wenye weledi wa hali ya juu. Aliendelea kwa kuwasisitiza Msimamizi msaidizi aweze kuuliza pale asipo elewa na siyo kujifungia na kitu ambacho hajakielewa vizuri na kuweza kuleta taaruki kwenye zoezi hilo muhimu la Uchaguzi.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe.Simoni Chacha aliudhuria katika mafunzo hayo na kuwapongeza wataalumu mbalimbali walioteuliwa katika nafasi ya Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata na Vijiji na kuwataka wa zingatie maadili na kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi na siyo kuendeshwa na akili na maamuzi binafsi.
Aidha Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndg.Abdul Kasembe aliwaeleza kwa kina wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata na Vijiji juu ya Sheria,Taratibu na Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwapitisha maeneo muhimu yote yanayo husiana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kutumia Muongozo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.