Katika hatua ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Mkuu wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe, Dkt. Wilfred Rwechungula,amefanya kikao maalum na wasimamizi wa vituo vya afya na zahanati. Kikao hiki kimelenga kuwakumbusha wajibu wao katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za uhakika.
Miongoni mwa mada zilizoshirikishwa katika kikaohicho ni pamoja na umuhimu wa kujaza taarifa za wagonjwa kwa usahihi ilikuepuka makosa yoyote. Aidha, wasimamizi wamepewa mafunzo ya ziada kuhusu utoaji wa huduma za UKIMWI, kufuatilia viashiria vya maradhi, na kuhakikisha kuwa watu wanaoishi na UKIMWI wanapata matibabu na huduma bora. Vilevile, sualala kuzuia maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto limepewa uzitomkubwa.
Aidha, kikao kimegusia Mada nyingine muhimu iliyojadiliwa ni matumizi sahihi ya kadi za watoto na wajawazito. Pamoja na umuhimu wa kadi hizi katika kufuatilia afya ya mama namtoto, wasimamizi wametakiwa kuhakikisha wanazitumia vizuri na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu manufaa yake.
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Rwechungula amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wasimamizi na watendaji wengine wa afya ili kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma anayostahili kwa wakati. "Tunataka kuona wananchi wetu wakiwa na afya njema, na hilo halitawezekana bila juhudi za pamoja," alisema Dkt. Rwechungula.
Kwa upande wao, wasimamizi wa vituo vya afya wameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa katika kikao hicho.Wamebainisha kuwa wataendelea kujitahidi kuboresha huduma zao ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata afya bora.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.