Benki ya NMB Tunduru kwa kushirikiana na mamlaka ya Mapato Tanzania TRA tawi la Tunduru na Bodi ya korosho wamefanya warsha ya kujadili changamoto zilizojitokeza katika uuzaji wa zao la korosho wilayani Tunduru katika mfumo wa stakabadhi ghalani katika msimu wa mwaka wa 2017/2018 ambapo malipo yalifanywa kwa njia ya Benki tofauti na miaka ya nyuma ilivyokuwa wakulima kulipwa fedha zao mikononi.
Warsha hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika, viongozi wa serikali, chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU), wawakilishi wa Bodi ya korosho, meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania tawi la Tunduru na menejenti ya benki ya NMB kanda ya kusini ambao ndio waandaji wa warsha hiyo.
Akizungumza katika warsha hiyo kaimu meneja kanda ya kusini Bi. Janeth Shango aliwashukuru wananchi wa wilaya ya Tunduru kwa kuchagua benki ya NMB kupisha malipo ya fedha zao kwani zitokanazo na zao la korosho, kwani ni zaidi ya shilingi bilioni 79 zimetishwa katika benki ya NMB tawi la Tunduru.
Meneja wa Benki Tawi la NMB Tunduru Ndg Goodluck Shirima akitoa elimu ya mikopo kwa wakulima katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa klasta ya Mlingoti ya kujadili changamoto zilizojitokeza katika uuzaji wa zao la korosho wilayani Tunduru katika msimu wa mwaka 2017/2018
Meneja wa NMB kanda ya Kusini Bi shango alisema kuwa changamoto kubwa iliyojotokeza katika ulipaji wa fedha za wakulima katika msimu huu ni kukosemna kwa uaminifu miongoni mwa wakulima waliokuwa wanatumia akaunti moja kuchulipwa kwani walijitokeza waliodai malipo mara mbili wakati wameshalipwa tayari.
Vilevile taarifa za kibenki kwa baadhi ya wakulima kutofautina na zile zilizopo katika vyma vya msingi hivyo kuleta usumbufu mkubwa sana, alisema unakuta mkulima anaitwa Juma saidi Issa lakini jina la akaunti Benki ni Saidi Issa.
Naye mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera aliviagiza vyama vyote vya msingi vya Ushirika wilayani Tunduru ambavyo bado hawajalipa fedha za wakulima kufanya malipo hayo ndani ya muda wa wiki moja tofauti ya hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Picha ya pamoja ya viongozi wa viongozi wa vyama vya msingi na menejementi ya benki ya NMB Kanda ya kusini baada ya warsha ya majadiliano ya changamoto zilizojitokeza katika msimu wa mwaka 2017/2018 na njia za kuzitatua katika msimu ujao wa mauzo ya zao la korosho wilayani Tunduru.
"naagiza wakulima wote ndani ya wiki moja wawe wamelipwa fedha zao za mauzo ya korosho ya msimu 2017/2018, kwa chama chochote kitakachokiuka maagizo hayo viongozi wake kuanzia mwenyekiti, na viongozi wa ngazi ya chini yake watachukuliwa hatua za kisheria"alisema mkuu wa wilaya Tunduru Juma Homera.
Juma Homera alitanabaisha kwamba ni vyema kwa benki ya NMB kusogeza huduma zake kila Tarafa kwa kufungua matawi na kuongeza vituo vya ATM (mashine za kutolewa fedha) pamoja kuanzisha (NMB mobile car) na kuboresha huduma za kibenki kupitia simu (NMB mobile) ili kupunguza msongamano kwenye benki iliyopo.
Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania tawi la Tunduru Ndg Joshua Mwakatumbula akitoa elimu ya mlipa kodi katika warsha hivi leo wakati wa majadiliano
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.