WANUFAIKA WA TASAF WAIPONGEZA SERIKALI
Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Tunduru waipongeza serikali kwa kuendelea kutoa ruzuku.
Hayo yamesemwa na wanufaika wa kaya maskini katika kijiji cha Chiuongo kilichopo kata ya namasakata wilayani wakati wa kupokea ruzuku awamu ya ishirini mapema wiki hii.
Akizungumza wakati wa mkutano na walengwa muwezashaji kutoka wilayani ndg chrisantus Haule alisema kuwa ni vyema walengwa kutimiza masharti ya mradi ikiwa ni Elimu, afya na kujikwamua kiuchumi.
Ndg Haule aliendelea kuwasisitiza walengwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanahudhuria masomo na wanasoma vizuri na kuwa na maendeleo bora katika Elimu.
Alisema pia ni muhimu kwa mama wajawazito kuhudhuria kliniki, na kujaza fomu za masharti za afya na Elimu ili kuepuka changamoto zinazowakabili wanufaika kutokana na kukosekana kwa taarifa sahihi.
Aliwataka wanufaika kujenga tabia ya kuanzisha miradi ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.
Kwa upande wake ndg Rashidi Abdallah Ngoma alishukuru serikali kwa kuwa ruzuku ya Tasaf imemsadia kuweza kuwapeleka watoto shule,kununua mbuzi wawili na kula vizuri pamoja na kupata mavazi bora.
"Naishukuru sana serikali kwa kuanzisha mpango huu, na ninaweza kusomesha na kupata mahitaji yangu ya kila siku"
mbuzi wa mzee Rashidi Abdallah Ngoma alionunua baada ya kupokea ruzuku ya Tasaf III kwa awamu 20
Naye bwana Ali Salum Nusura alisema kuwa wanufaika wamekuwa wanakosa ruzuku za wanafunzi walioko shule za msingi na hasa wananfunzi wa sekondari wamekua wakikosa ruzuku hiyo kila yanapofanyika malipo.
"Nina watoto watatu lakini hawapati ruzuku ya Elimu na fomu za masharti nimejaza zipo wilayani" alisema Rashidi.
Hata hivyo wananchi wa kijiji cha Chiungo waliambiwa wawe na subira kwani malalamiko yao yanafanyiwa kazi ngazi ya wilaya.
Imetolewa
Kitengo cha Tehama na Uhusiano
Halmashauri ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.