Mpango wa Kunusuru kaya Maskini Wilaya ya Tunduru ambao mpaka sasa una jumla ya kaya 20,869, kati ya hizo kaya jumla ya wanufaika wapatao 3,745 wamehitimu katika mpango huo baada ya miaka 10 ya kuingia kwenye mpango huo na kunufaika.
Akizungumza na wanufaika waliohitimu na wanaoendelea kwenye mpango wa TASAF katika kijiji cha Misufini na Namiungo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Simon Chacha aliwapongeza wale wote walioutumia mpango huu kujiimarisha kiuchumi huku wakizitumia fedha walizowezeshwa kufanya shughuli za maendeleo.
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Simon Chacha
“Mnapoingia TASAF mjipange na kutoka pia, kwa maana ya kwamba kile mnachowezeshwa kiwasaidie kujikwamua kutoka katika hali ngumu ya kiuchumi” Alisema Mhe. Chacha “Nitahakikisha malipo ya wanufaika yanakamilika na yanawafikia kwa wakati walengwa wote wanaoendelea na Mpango huu”.
Mhe. Chacha aliendelea kusema anaamini wahitimu hawa watatumia ujuzi na maarifa waliyopata kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao. Na kuwatakia kila la kheri katika juhudi zao za kimaendeleo.
Kwa upande wake Afisa ufuatiliaji wa Wilaya ya Tunduru kutoka makao makuu ya TASAF ambayo yapo Dar es salaam, Bw. Lazaro Mapimo aliwashukuru na kuwapongeza wanufaika ambao wamehitimu kwenye mpango, huku akiwaomba waendelee kusimamia miradi ambayo ilitokana na TASAF, ili iweze kuwasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali na kuwasisitiza kuzingatia lishe bora na kuwapeleka watoto shule.
Pichani ni Afisa ufuatiliaji wa Wilaya ya Tunduru kutoka makao makuu ya TASAF Bw. Lazaro Mapimo
Wanufaika waliohitimu kwenye mpango wameshukuru sana, kwani mpango huu umewawezesha wamepata fursa ya kuboresha maisha yao na familia zao kupitia mafunzo na msaada wa kifedha waliyopata kutoka kwa mpango huo.
Imetolewa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru,
Orpa Kijanda,
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.