Wanawake Wasisitizwa Kuwa Walimu wa Maadili Katika Familia
Mwakilishi wa Mbunge wa Kusini Mhe. Saidi Bwanali amewataka wanawake kusimamia maadili, hasa katika familia, wakati akizindua maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Wilaya ya Tunduru.
Akizungumza baada ya kuwasili katika uzinduzi huo, Mhe. Bwanali alisisitiza umuhimu wa Wanawake kutambua haki zao na wajibu wao kama nguzo imara katika familia na jamii.
Mhe. Bwanali pia alihamasisha wanawake kuwa na ujasiri wa kuthubutu kugombea nafasi mbalimbali hasa za uongozi kwani mwanamke ni nguzo imara katika jamii.
"Jambo lolote ambalo Mwanamke atalishika, atalisimamia kwa ufasaha na kuhakikisha linafanikiwa." Alisema Mhe.Bwanali.
Aliwataka wazazi, hasa akinamama, kuwapa Watoto malezi bora na maadili mema, ikiwemo Elimu ya Dini, itakayowasaidia kujenga maisha yao bora sasa na baadaye.
Katika Hafla hiyo ya Uzinduzi wa Siku ya Mwanamke Duniani Ofisi ya Maendeleo ya Jamii ikishirikiana na Wanawake Wilaya ya Tunduru walitoa Msaada kwa watu wenye amahitaji Maalumu.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatafanyika Machi 08 2024,ambapo Mkoa wa Ruvuma Yataadhimishwa katika Wilaya ya Mbinga.
Kaulimbiu ya siku ya wanawake Duniani kwa mwaka huu ni "Wekeza kwa Mwanamke: Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii."
Kauli hii ikiwa inalenga katika kuhisihi jamii kuwekeza kwa mwanamke na kumuamini, kwani mwanamke ameonekana kuwa ni nyezo muhimu sana katika jamii ana uwezo wa kushiriki katika kila jambo la maendeleo.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wanawake kutoka maeneo mbalimbali Wilaya ya Tunduru na mashirika ya kijamii
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.