WANAWAKE TUNDURU WAAZIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Wanawake Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wafanya madhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kila ifikapo march 8 hufanyika madhimisho haya ,na kimkoa yalifanyika wilaya ya Mbinga na kuwakutanisha wanawake wa mkoa mzima
Akizungumza katika madhimsho hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma jecelyne mganga alisema haya madhimisho yalitakiwa yafanyike kiwilaya tarehe 6/3/2024 ila kutokana na changamoto ya msiba wa taifa ndio ikawa tarehe 10 /3/2023
Jecelyne alisema madhimisho haya yanakwenda kwa kaulimbiu ya mwaka 2024 ,WEKEZA KWA WANAWAKE KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII
Pia Diwani wa viti Malumu kutoka tarafa ya Matemanga Stawa Timamu ambaye ni mwenyekiti wa huduma za jamii alisema wanawake wanatakiwa kusimamia maadili ya kitanzania ,amewataka wanawake wapunguze ukatili wa kijinsia
Aidha JUWATU SACCOS wilaya hapa wakati wakisoma Risala fupi walisema wamefanikiwa katika Nyanja toufauti ,wamesajiliwa na wana milioni 31 , alisema mtaji umeongezeka na saccos hiyo imesajiliwa na Afisa ushirika wilaya ya Tunduru na wanajivunia mafanikio hayo
Mgeni Rasmi katika Hafla Bi. Sabina Lipukila amesema, Mwanamke anathamani kubwa katika jamii inayomzunguka, amewataka wananwake kutoendeleza zana ya kumuona mwanamke mwingine ni adui,
Aliendelea kuwasihi wanawawake hasa wazazi , kuwa na malezi bora kwa watoto wao hasa wakike , amewataka kuwaelekeza watoto wao katika njia ya kumtegemea Mungu, na kuwataka wazazi kuwapa watoto wao Elimu ya Dini.
“kupitia kauli mbiu hii ya siku ya Wanawake , inatutaka wanawake kuwajibika katika jamii zetu”, “Watoto wetu wa kike tuwape thamani kubwa na tuwaelekeze katika Elimu ya Dini”. Alisema Bi. Lipukila
Bi. Lipikila, Amewasisitiza wanawake kuwa na uthubutu katika kushika nyazfa mbalimbali serikalini na ata katika jamii inayowazunguka ili kuharakisha maendeleo ya Taifa na hata Maendeleo ya jamii wanaishi.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Wanawake Duniani yanaadhimishwa kila mwaka Machi 08, ambapo Chimbuko lake ni huko marekani Miaka ya 1900 kwa wafanyakazi wa sekta ya Viwanda kupinga mazingira mabovu ya kufanya kazi.
“Wekeza kwa mwanamke, : kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.