Hayo yamesemwa na mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg.Gasper Zahoro Balyomi kabla ya kukabidhi hundi ya 103,112,284.00 ikiwa ni awamu ya tatu utekelezaji wa utoaji wa mkopo wa kisheria wa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa vikundi 37 vya wanawake 14, vijana 14 na watu wenye ulemavu vikundi 9.
Halmashauri inaendelea kuwawezesha wanawake ili kuweza kujiinua kiuchumi na itawasimamia katika kuhakikisha kuwa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inakuwa endelevu kwa kipindi chote atakachokuwa akitoa huduma katika halmashauri ya Tunduru,.
Naahidi kuendelea kuwaendeleza wanwake kiuchumi kwa kuwashika mikono kwa kutoa mikopo ya asilimia kumi katika mapato ya ndani, amesema "mimi kama mkurugenzi kupitia idara ya maendeleo ya jamii nitaendelea kuwainua wanawake kwa kuwa nimeona mnaweza na pia kupitia idara ya sheria nitahakikisha wanafika hadi vijijini na ile mifumo dume yote inayokandamiza wanawake inaondolewa kabisa"
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg.Gasper Balyomi (Kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani Milioni 103.1 kwa kaimu Mkuu wa wilaya ya Tunduru ambaye pia ni katibu tawala wilaya Ndg.Ghaibu Lingo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika uwanja wa baraza la iddi.
Akiongea katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kaimu mkuu wa wilaya ya Tunduru Ndg.Ghaibu Lingo baada ya kukabidhiwa Hundi na mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru kwa ajili ya kukabidhi kwa vikundi 37 aliwataka wanufaika wa mkopo huo kuutumia katika kujiletea maendeleo na sio kwenda kufanya shughuli ambazo ziko nje ya mpango kazi walioombewa ili kujikwamua kiuchumi na kutoa nafasi kwa vikundi vinginge kuweza kukopeshwa zaidi.
Aidha aliendelea kusema kuwa mkopo huo sio zawadi inayotolewa kwao bali wanatakiwa kurejesha kwa wakati ili kuongeza wigo wa utoaji mkopo kwa vikundi vingine vingi zaidi na kukuza uchumi wa wananchi kwa vikukndi na mtu mmoja mmoja.
Kimu mkuu wa wilaya ya Tunduru Ndg.Ghaibu Lingo akitoa maekelezo ya serikali kwa vikundi 37 vya walemavu, wanawake na vijana vilivyopatiwa mkopo na halmashauri katika siku ya wanawake duniani.
Pamoja na hayo Ndg.Ghaibu Lingo aliwataka wanawake kupendana na kutumia nafasi za uongozi walizonazo katika kuwainua wanawake wengine lakini pia kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwezi octoba 2020 ili kupingana na dhana potofu ya kugombea katika nafasi za viti maalum "twende tukagombee majimbo na sio kusubiria nafasi za kuteuliwa za viti maalum pekee kwani wanawake tukiungana tunaweza"
Nao wanufaika wa mkopo huo wa milioni 103.1 waliishikuru serikali ya Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kuendelea kuwashika mkono katika kuwakopesha mkopo usiokuwa na riba kwani umewatelea manufaa makubwa sana hadi kufikia sasa wengi wao wanamiliki biashara, kufuga kwa tija na vipato vya familia zao vimeongezeka ukilinganisha na awali ambapo hawakupata mkopo kutoka serikalini.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.