Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh. Wakili Julius S. Mtatiro, amefanya kikao kazi na watendaji Kata, waratibu wa Elimu Kata pamoja na Magavana katika maandilizi ya kupokea wanafunzi mwaka wa masomo 2024. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Klasta- Mlingoti tarehe 05.01.2024.
Pichani ni Watendaji Kata, waratibu wa Elimu Kata pamoja na Magavana wakiwa katika kikao kazi.
Katika kikao hicho Mh. Wakili Mtatiro aliwapongeza watendaji hao kwa kazi wanayoifanya katika kata zao, ya kuhakikisha suala la Elimu linapewa kipaumbele. Aliwataka waendelee kufanya kazi kwa bidi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaohitimu elimu ya msingi wanapata fursa ya kujiunga na Elimu ya Sekondari.
Mh. Wakili Mtatiro aliagiza kuhakikisha wanakutana na wazazi/walezi wote ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ndani ya siku tatu ambazo ni kuanzia tarehe 06-07 mwezi Januari 2024. Pia, aliwataka magavana kupeleleka taarifa ya idadi ya wanafunzi wote waliofauru kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka huu ifikapo siku ya jumanne, tarehe 09 Januari 2024.
“Vikosi kazi na Polisi kata wote waende kwenye kata zao, ili washiriki kikamilifu kwenye vikao vya wazazi na viongozi wa kata” Alisema Mh. Wakili Mtatiro “Miundombinu tumeikamilisha hivyo, ni wajibu wetu kusimamia na kuhakikisha vijana wanapata Elimu”
Aidha, Mh. Wakili Mtatiro alisisitiza kuwa zoezi hili linawapasa viongozi wote kuanzia ngazi ya kijiji, kata pamoja na magavana kushiriki kikamilifu, pia, aliagiza kuwa wazazi/walezi wote wataokaidi kupeleka wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2024, kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sharia haraka.
Akifunga kikao hicho Mh. Wakili Mtatiro alisisitiza kuwa Elimu ni haki ya kila mtoto, hivyo ni wajibu wa mzazi/mlezi kuwapeleka watoto wao shule. Aliwataka watendaji wote wanaosimamia sekta ya Elimu Wilayani Tunduru kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza yale yote ambayo Wizara na Serikali imeyawekea mikakati ili kuboresha Elimu nchini Tanzania. Alionya kuwa hakuna atakayeruhusiwa kukwepa wajibu huu.
Shule zote Wilayani Tunduru zinatarajiwa kufunguliwa na kuanza kupokea wanafunzi ifikapo Jumatatu ya tarehe 08 Januari mwaka 2024, hivyo wawazi/walezi wote wanaagizwa kupeleka wanafunzi wao ili wakaandikishwe kujiunga na elimu msingi na awali pamoja na Elimu ya Sekondari.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.