WANAFUNZI 1874 , kupata fursa vyuo ufundi Tunduru
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Wakili, Julius S. Mtatiro, amewakabidhi Wakuu wa vyuo vya ufundi Wilayani humo majina ya Wanafunzi ambao wanakosa sifa za kujiunga na kidato cha kwanza, cha tano na vyuo vya kati kwa mwaka 2024.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, ambapo kilihudhuriwa na Maafisa Elimu Msingi, Elimu Sekondari na Wakuu wa vyuo vya Ufundi Nandembo (FDC) ,Mbesa na Kiuma.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Maafisa wa Elimu ya Sekondari na Elimu ya Msingi wamesema majina 1,874 yamekabidhiwa, ambapo Wanafunzi 1,326 ni wa elimu ya sekondari na Wanafunzi 548 ni wa elimu ya msingi.
Hatua hii imefikia baada ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Wakili Julius S. Mtatiro kuwataka Idara ya Elimu Msingi na Sekondari kutambua majina ya wanafunzi hao waliokosa sifa ya kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza, kidato cha tano na vyuo vya kati kwa Mwaka 2024.
Ambapo hapo awali, alizungumza na wakuu wa vyuo hivyo kuweza kuwapatia nafasi kwa Wanafunzi hao ambao wanakosa sifa hasa za kujiunga na Elimu inayofata hasa kidato cha kwanza, kidato cha tano na Vyuo vya kati.
Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo, Dc, Mtatiro amewasisitiza wakuu wa vyuo hivyo kuyafanyia kazi majina hayo na kuandaa fomu za kujiunga na vyuo hivyo ili kuwawezesha Wanafunzi hao kuripoti mapema iwezekanavyo na kuanza masomo yao.
“Jambo hili linakwenda kuwa msaada mkubwa katika kumaliza tatizo la watoto wetu kukosa fursa”. Alisema Dc, Mtatiro “ kwani itakuwa nyenzo kubwa ya kutatua tatizo la ajira na vijana kuweza kujiajiri”.
Wakuu wa vyuo vya ufundi wamesema kwa nyakati tofauti kuwa, wako tayari kushirikiana kwa ukaribu katika kuwapokea katika vyuo vyao.
Hatua hii inatarajiwa kusaidia wanafunzi ambao hawakupata fursa ya kujiunga na elimu ya juu kupata elimu ya ufundi na kujiajiri.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.