JESHI la Polisi mkoani Ruvuma, linawashikilia watu watano wa Kijiji cha Magwamila Songea Vijijini kwa kosa la kumiliki Silaha ya kivita aina ya AK 47.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jana,Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa alisema, tukio hilo lilitokea taerehe 15 mwezi huu huko mto Ruvuma.
Kwa mujibu wa kamanda Maigwa, Fidel Mangala(20) alikutwa na silaha hiyo na katika mahojiano ya kina aliwataja wenzake ambao anashilikiana nao katika kufanya uharifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma na Nchi jirani ya Msumbuji.
Kamanda Maigwa aliwataja watuhumiwa wengine ni Maulid Jafar(45) mkazi wa Kijiji cha Nambendo, Maganga Msoma mkazi wa Nambedo na Shame Omari(45)mkazi wa Nchi jirani ya Msumbiji ambaye yupo Magereza kwa kosa la kupatikana na silaha nyingine ya kivita aina ya AK 47.
Aidha kamanda Maigwa alisema, baada ya mahojiano ya kina watuhumiwa hao waliongoza hadi eneo walikoficha silaha hiyo ambayo walifukia Ardhini na baada ya kufukua eneo hilo ilipatikana silaha moja ya kivita aina ya AK 47 pamoja na risasi sita ndani ya magazine.
Kamanda huyo wa polisi alieleza kuwa, watuhumiwa hao wote walikiri kujihusisha na uwindaji haramu na matukio mengine ya uharifu ndani ya Tanzania na Nchini Msumbiji kwa muda mrefu.
Hata hivyo Kamanda Maigwa alisema, katika kufuatilia mtandao wao wa ujangili pia walifanikiwa kuwakamata watu wawili Issa Millanzi(46) na Fidel Mangala(20)wakazi wa Kijiji cha Nambendo Songea vijijini wakiwa na meno mawili ya Tembo yenye thamani ya shilingi Ml34.5 ambayo waliyahifadhi kwenye mfuko wa Sulphate na kuyafikia ardhini katika shamba la Issa Musa.
Kamanda Maigwa aliwaeleza waandishi wa Habari kuwa,watuhumiwa hao walikiri kuwa silaha hizo ndizo walitumia kuulia tembo na kupata meno hayo.
Amewataka wakazi wa mkoa wa Ruvuma kwa wale wanaomiliki silaha kinyume na sharia wazisalimishe haraka iwezekanavyo na kuwataka waache kujihusisha na uwindaji haramu n ahata matukio ya kiharifu kwani Jeshi la Polisi limejipanga kikamiifu na halitasita kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na matukio ya uharifu.
MWISHO
ReplyReply allForward |
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.