Kufuatia usumbufu kwa wakulima wengi wa zao la Korosho juu ya malipo yao, wamekuwa na malalamiko mengi sana ambayo yamekuwa yakiwakilishwa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupitia Idara ya Kilimo na Ushirika kwa kushirikiana na chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU).
Wakulima wengi wamekuwa wakilalamika kutokulipwa na wengine malipo yao kucheleweshwa kutokana na sababau mbalimbali ikiwemo ya muongozo wa serikali wa kutaka kila mkulima kufungua Akaunti benki ndipo aweze kulipwa.
Aidha ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru amekuwa akitatua changamoto hizo kila wakati na kuwaisadia wakulima kupitia idara ya kilimo na ushirika kupata msaada awa njia bora za kuweza kupata malipo yao ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti benki kwa kila mkulima ili haki iweze kutendeka.
Mkulima Ndg Saidi kutoka Kata ya Mchuluka anayedai kutokulipwa malipo yake ya mnada mmoja hali ambayo sio kweli baada ya uchunguzi kufanyika katika taarifa za chama cha Msingi Nakatete.
Akiendelea kutoa changamoto za wakulima mbalimbali wanazowasilisha afisa ushirika wilaya Ndg Peter Malekela amesema kuwa wakulima wengi wamekuwa na madai ambayo kwa uhalisia yanakuwa haya ukweli ndani kutokana na uelewa mdogo wa matumizi ya malipo ya kutumia benki.
Akitolea mfano wa mkulima Ndg Saidi kutoka Kata ya Mchuluka ambaye anadai kutolipwa fedha zake kwa baadhi ya Minada wakati ameshalipwa fedha zake zote baada ya uhakiki uliofanywa na Ofisi ya Ushirika kupitia chama cha Msingi Nakatete.
Afisa Ushirika wilaya alikemea kwa vikali sana tabia ya baadhi ya wakulima kutoa taarifa za uongo kwa uongozi wa wilaya ya kutokulipwa fedha zao ilihali wameshalipwa kwani endapo itabainika mkulima anaidanganya serikali ili kulipwa mara mbili atachukuliwa hatua za kisheria.
Hii ni stakabadhi ambayo aliiwakilisha Mkulima kutoka kata ya Mchuluka Amcos ya Nakatete aliyoiwasilisha katika Ofisi za Ushirika wilaya kudai malipo ambayo tayari alishalipwa.
Na kwa upande wa mwenyekiti wa chama cha msingi Amcos ya Nakatete Ndg Kimaro alisema kuwa anakumbana na idadi kubwa ya wakulima kudai malipo mara mbili mbili na baadhi ya wakulima wenye kiwango kidogo cha mazao chini ya kilogram hamsini wanakuwa wasumbufu sana.
alisema Kimaro "wakulima hawa wamekuwa wasumbufu sana kiasi kwamba hata kufungua akaunti hawataki lakini wanataka malipo yao na ndio kwa asilimia kubwa hawajalipwa fedha zao na wengine kupitisha fedha kwenye akaunti za watu wengine hali inayoleta utata mkubwa"
Akizungumzia suala la mfumo wa malipo Ndg Kimaro alisema kuwa anaishauri serikali kupitia bodi ya zao la korosho kuona namna nzuri ya kuwalipa wakulima wanaokuwa na uzalishaji mdogo na kutoa elimu zaidi ili wakulima wengi waweze kufungua akaunti.
pia aliendelea kusema kuwa wakulima wengi wamekua na tabia ya kutoa fedhazao zote wanapokuwa wanalipwa hivyo baada ya kuzitumia na kwisha wanaanza tena wanajisahau na kuona kana kwamba hawajalipwa fedha zao hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwenye vyama vya msingi na Halmashauri kwa ujumla.
"madai mengine wanayodai wakulima yana uhalili kwa sababu kuna ambao bado hawajalipwa mpaka sasa ambao majina yao yametoka na yamebandikwa katika mbao za matangazo katika vyama vyo vya msingi kwa ajili ya kulipwa fedha zao tayari" alisema Ndg Kimaro
wakulima mnaombwa kuzingatia sheria, kanuni na Taratibu ili kuweza kupata haki zao ikiwa ni pamoja na kulipwa fedha za korosho, hivyo miongozo inayotolewa na serikali ni vyema ikazingatiwa ili kuiendeleza wilaya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.